Sunday, March 28, 2010

Sala kabla kula chakula + Jumapili njema kwa wote!!

Kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu, Utubarikie Mungu wetu sisi na chakula chetu tupate nguvu ya kukutumikia vema Amina. NAWATAKIENI WOTE AMANI KATIKA JUMAPILI HII YA MATAWI NA YA 13 PIA YA MWISHO YA MWEZI HUU MACHI NA WOTE MNAPENDWA!!


15 comments:

  1. Yani umenitamanisha mate yananitoka hapa chakula cha nyumbani hicho.

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana.

    Bora umenikumbusha, wacha niende sokoni fasta nami mchana nile ugali samaki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usisahau kununua mabenda uteremshe nayo

      Delete
  3. Duuuuu,huo ugali na samaki umenifanya mate yanidondoke,Jumapili njema kwako pia.

    ReplyDelete
  4. Mmh,da Yasinta, sijala ugali siku nyingi!Natamani!

    ReplyDelete
  5. niko wazaliwapo samaki japo sio mshiriki wa kitoweo hiki

    acha ubaguzi Yasinta juu yawatu wa jumapili na matawi, kuna tuusiokuwa na siku maishani yaani siku zote kwetu ni sawa na zinalingana

    ReplyDelete
  6. Yasinta, tueleze kama kweli uliandaa mwenyewe au ni picha uliyopiga siku uliyoenda kule Songea kwa likizo. Hapo ughaibuni unga mweupe kama huu upo kweli?

    ReplyDelete
  7. Mmmmmhhhhh!!!!
    Ni dhambi kutamani na naamini KUTAMANISHA PIA.
    Sasa jumapili hii watuambia tusali huku ukitutamanisha na li-nguna kwa samaki. Sijui tusipo-concentrate kwenye sala sababu ya taswira hiyo, dhambi zitabebwa na nani?

    Mama ntilie wanajua kupika jamani, nakumbuka nilivyompeleka Yasinta kwa Mama Tatu aka-oda huo ugali na kupiga picha. Nilidhani uliipoteza. Kumbe liitunza?
    Duh

    ReplyDelete
  8. Mmmm! Yasinta umenitamanisha ugali na samaki sijala siku nyingi sana,kwanini lakini?unatutamanisha vitu wengine sio rahisi kuvipata.

    Jumapili njema na kwako pia.

    ReplyDelete
  9. Safi sana hii, kabla ya kula lazima kusali, katika maadili ya kikristu.

    ReplyDelete
  10. katika sala zoote naipenda hii maana ni fupi. tofauti na zile za wengine mpaka wanaanza kuombea mkulima, mvunaji, mpishi. wanaombea amani kisha chakula.

    ReplyDelete
  11. Hebu nifundisheni sala nyingine ya kuombea chakula isiwe hiyo hapo juu

    ReplyDelete