Monday, February 15, 2010

Salaam za makabila yetu

kijijini kwetu
Wasomaji wapendwa wa blog hii, najaribu kufanya utafiti wa lugha za makabila yetu hapa nchini. Kwa mujibu wa tafiti inasemekana kuna makabila zaidi ya 120 hapa nchini.Niliamua kuangalia zaidi salaam, hususan za asubuhi, Kutokana na utafiti wangu nimepitia makabila kadhaa na kukutana na maneno yanayotumiaka katika salaam za asubuhi ambayo yanafanana kidogo, hebu tuone maneno hayo ni yapi:




KINGONI: Uyimwiki = Habari za asubuhi


KIZIGUA: Kugona vihi = Habari za asubuhi


KINYAKYUSA: Ughonile = Habari za asubuhi


KIYAO: kwimukaga = Habari za asubuhi


KIPARE: Murevuka = Habari za asubuhi


KIUNGUJA: wambaje = Habari za asubuhi


KISAMBAA: Onga makeo = Habari za asubuhi


KIANGAZA: Mwalamtse = Habari za asubuhi


KINYAMWEZI: Mwangaluka = Habari za asubuhi


KICHAGA: Shimbonyi = Habari za asubuhi


KIMERU: Konumbware = Habari za asubuhi


KIMASAI: Sopai = Habari za asubuhi


KISUKUMA: Mwadila = Habari za asubuhi


KIHEHE: Kamwene = Habari za asubuhi


KIBENA: Kamwene = Habari za asubuhi


KIKINGA: Ulamwihe = Habari za asubuhi


KINYIRAMBA: Ulalaliani = Habari za asubuhi


KIHAYA: Wabonaki = Habari za asubuhi




Kwa leo naishia hapa mwenye nyongeza anaweza kuongeza ili tujifunze pamoja.
Tukutane wakati ujao


Mada hii nimeichukua kutoka kwenye kibaraza cha VUKANI cha dada Koero, nami nimevutiwa nayo nikaona sio vibaya kuirejea ili kujikumbusha.

17 comments:

  1. KIGOGO - Mbukwenyi = Habari za asubuhi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mambo bidada naomba nitafute

      Delete
    2. Kisukuma sio mwadila ni ng'hwangaluka / ng'hwadila inatumika jioni na sio salamu ya asubuhi

      Delete
  2. Ahsante sana. Maana nyingine sikuwa nikizifahamu.

    ReplyDelete
  3. Halafu we Yasinta, hiyo Mwadela na Mwangaluka ya kinyamwenzi na kisukuma kuna ka utata hapo hebu Ng'wanambiti tusaidie kidogo hapo. Maana mi nimeolewa huko usukumani lakini asubuhi twasalimiana mwangaluka na kama hamjaonana kitambo then tunasema mwadela.

    ReplyDelete
  4. MMhm, lugha ya Kiunguja ndio lugha ya kabila gani vile?

    ReplyDelete
  5. Lulu, uminisalimia? Mbukwaaaaaaaaa!


    Kuna ka ukweli kabsaa katika hilo kwa kuwa kwa wasukuma asubuhi huwa ni MWANGALUKA (ng'wangaluka) na Mwadila (Ng'wadila) hutumika kuanzia saa 6 nchana!

    Kwa kikurya 'Bhwakeye ama Waraye'

    Lulu, bhalamsaje bhose...lol

    ReplyDelete
  6. Kazi kubwa umefanya. Si wajua lugha za watu, matamshi ndio taabu
    Wasukuma na wanyamwezi salamu zao zinakaribiana sana!
    Nimeishi umasaini miaka 2, sopai ni salamu ya wakati wowote, na unajibu sidai, matamshi ni fasta sio kama lilivyoandikwa, kwa msisitizo unaweza kusema sidai nalle!
    Kwa wahaya wajua lugha watasaidia, lakini hutamkwa tofauti kidogo.
    Waangaza nafikiri wanasalimiana waramutse, copyright na kinyarwanda!
    Wahadzabe, DUH, Siwezi kuandika, maana salamu haiandikiki vizuri maana sauti inatoka kama mtu atakaye kutema koozi, yaani inatamkiwa kooni, nilipokuwa Singida tulikuwa tunasalimiana kinyaturu kwa kusema habari ya Diu, labda spelling ndo tatizo, na kinyiramba sijui inaandikwaje, lakini tulikuwa tunasema ulailiani!
    Wakara na wakerewe, ukichanganya na wajita, wakwaya nk salamu za wanaume na wanawake zinatofautiana, na pia watu wa rika moja wanaume na wanawake zinatofautiana, ila naona nafasi haitoshi hapa, na sie matatizo ya kuishi sehemu nyingi na makabila tofauti tunaishia kuchanganyikiwa DUH! Watu wa kijiweni salamu zao za asubuhi wakati mwingine hawajasukutua midomo.. salamu zikimwagika zinakuwa kama siweji vile!

    ReplyDelete
  7. Acha hizo, nani kasema Wabonaki ni hazari za asubuhi?
    Lione vile

    ReplyDelete
  8. kiunguja hakuna wambaje

    habari za asubuhi hiyo wambaje ni ya wapi

    ReplyDelete
  9. kikwetu

    ugonile = umeamkaje
    utwa lubunju = habari ya asubuhi
    mulibakafu = hamjambo
    utwa mbombo = habari ya kazi
    utwa 'masiku = habari za siku

    ReplyDelete
  10. Jamani Yasinta usiwasahau na ndugu zako wayao.
    Kuimukaga=habari za asubuhi/umeamkaje
    Habari chi=habari gani
    Z.

    ReplyDelete
  11. Za bwankya- za asubuhi iko ndo kihaya sasa

    ReplyDelete
  12. KIJALUO -OYAWRE ndio salaam yenyewe,ichiew nade ni neno endelezo baada salaam.

    ReplyDelete
  13. nani kakuambia kuwa kimeru ni kwanumbware hiyo ni umesemaje za asubuhi kwakwimboare

    ReplyDelete
  14. Naombeni kujua happy birthday kwa kinyakyusa inasemwaje?

    ReplyDelete