Sunday, December 13, 2009

Ni Jumapili ya tatu ya majilio:- Ngoja tusali Sala ya Wazazi wakiwaombea Watoto wao

Tunawaangalia , Ee Bwana
Hawa uliotujalia.
Katika hawa tunajiona sisi wenyewe.
Je, kweli tulikuwa hivi sisi
Tulipokuwa watoto?

Tulipigana hivi?
Tulipaga kelele hivi?
Tulileta furaha namna hii
Na mateso namna hii kwa wazazi wtu?
Tunashangaa na kujiuliza....

Tunajaribu kukumbuka-----
Kukumbuka jinsi ilivyokuwa
Tulipokuwa watoto wadogo bado
Tukiwatazama watu wakubwa.

Wakati mwingine wanatutia wasiwasi, Bwana.
Au kwa namna nzuri zaidi, tunajitia wasiwasi sisi wenyewe
Kwani si rahisi kuwa sawa daima.

Lakini kuna furaha pia,
Furaha kubwa wanayotuletea;
Nao hutufanya tuone fahari,
kwani ni watoto wema.

Tunakushukuru kwa ajili yao Bwana,
Wao ndiyo zawadi yako bora kwetu,
baada yetu sisi wenyewe.

Utusaidie
tuunganisha mikono yetu na mkono yako
Ili, Ee Baba,
Wawe kweli
Watoto wetu.
Amina.
JUMPILI NJEMA KWA WOTE

4 comments:

  1. Ameni kwa aliyefanikisha kalenda hii KUWA MAARUFU ambayo inafanya MPAKA wajanja wana mpaka siku waiitayo JUMAPILI!:-(

    ReplyDelete
  2. Ameni mungu atinde atuongezee maisha marefu tuweze kuwalea watoto wetu

    ReplyDelete
  3. fanikisha sala yasinta MUNGU akubariki dada...

    ReplyDelete
  4. Natumaini wote mlikuwa na jumapili njema binafsi nilikuwa na wakati mzuri. Niliitumia j´pili yangu kwa kumwangalia binti yangu akicheza "handboll" Asanteni wote

    ReplyDelete