Kila mtu akiulizwa ni mwanamke gani maarufu au aliye ngangari zaidi, kama anatafakari vizuri, atasema kuwa ni mama yake, hasa kama alimlea kwa uadilifu. Pengine mwingine atasema ni mkewe, kutegemea na namna wanavyoishi kwenye uhusiano wao wa kindoa.
Lakini, linapokuja suala la mwanamke ambaye hakuhusu, ambaye unaamini au kudhani kwamba, ndiye ngangari zaidi hapa duniani, hasa katika siasa na uchumi, inaweza kuwa mtihani mgumu kwako kutoa jibu sahihi.
Ni kweli, unaweza kutoa jibu, lakini siyo lazima jibu lako liwe sahihi.
Kama ni sahihi, itakuwa ni kwa sababu tu, unamjua huyo uliyemtaja, na wengine huwajui.
Hivi ndivyo ambavyo imetokea kwenye kura iliyofanyika ya kuwataja wanawake wanaodhaniwa kuwa maarufu hapa chini ya jua kwenye nyanja ya siasa na uchumi.
Karibu kila Mtanzania angetarajia kuwa wakitajwa wanawake 100 duninai ambao ni maarufu kwa sasa, huenda Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro angetajwa. Matarajio hayo yangetokana na sababu mbalimbali.
Kwanza, unaibu wa Katibu Mkuu wa UN, siyo nafasi ndogo hapa duniani. Pili, kwa mwanamke kutoka Afrika tena kwa nchi ambayo ni miongoni mwa zile maskini kabisa, kushika nafasi hiyo, ni jambo la kinasibu zaidi kwa mitazamo ya mgawanyo wa dunia. Tatu, ingetarajiwa naibu atoke angalau bara Amerika, kwani Katibu Mkuu anatoka Asia, bara maskini karibu sawa na Afrika kwa uwiano.
Kwa bahati mbaya, jarida maarufu duniani kwa kufanya tathmini za viwango mbalimbali kuanzia utajiri, uzuri na umaarufu wa binadamu, la Forbes linaonesha katika taarifa zake za wiki mbili zilizopita kwamba, Migiro hayumo kwenye orodha ya wanawake 100 maarufu duniani katika nyanja za uchumi na siasa.
Kutoka Afrika ni wanawake wawili tu walio kwenye orodha hiyo. Kwanza ni , Waziri Mkuu wa Msumbiji, ambaye anashikilia nafasi ya 89 diuniani kwa umaarufu. Halafu anafuatiwa na Rais wa Liberia, , ambaye anashikilia nafasi ya 100.
Hii ina maana kwamba, Waziri Mkuu wa Msumbiji ni maarufu zaidi duniani, ukilinganisha na Rais wa Liberia, , nchi iliyoweka historia duniani kwa vurugu kubwa za kisiasa, zilizopelekea marais wawili kuuawa kinyama na mmoja kupamba vyombo vha habari dunia kuhusiana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Rais Ellen Johnson ndiye Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika, lakini anakuwa Rais baada ya uchaguizi huru na wa haki uliofuatia umwagikaji wa damu nyingi ya kutosha. Bado huyu anashikilia nafasi ya 100, wakati Waziri Mkuu wa Msumbiji anashikilia nafasi ya 89!
Hapa ndipo ambapo matokeo haya ya jarida la Fobes yanatia mashaka. Ni kweli kwamba, uchaguzi huo umefuatia kura kutoka kwa watu duniani kote.
Bahati mbaya ni kwamba, kura hizo kwa sehemu kubwa zimehusisha matumizi ya vyombo vya kisasa ambavyo havipo kwa wingi Afrika, hasa mtandano wa intaneti.
Katika orodha hiyo kuna majina ya wanawake ambayo huenda kwa umaarufu, akili ya kawaida inaweza kukuonesha kwamba, hawawezi kumzidi Asha Rose Migiro. Hebu kwa mfano, tuchukulie mwanamke kama , ambaye ni mtendaji kuuu wa Benki ya Leumi ya Israeli. Je, huyu mama uliwahi kumsikia au hata kumsoma kwenye chombo chochote cha nje? Huyu anashikilia nafasi ya 83 kwa umaarufu.
Huenda inabidi Afrika nayo sasa iwe na utaratibu wa kutafuta maoni ya dunia nzima ambapo waafrika nao watashiriki sawa kusema kuhusu nini wanaona, sawa na watu wengine duniani. Inaonekana wazi kwamba, hata viwango vya umaskini vinavyopangwa kutoka Ulaya na Marekani ni kwa vigezo ambavyo havifutu na kukidhi ukweli mkubwa zaidi unaowahusu Waafrika.
Kwenye orodha hiyo, inaonekana kuwa, Rais wa Ujerumani, , ndiye mwanamke maarufu zaidi duniani. Wu yi, ambaye ni makamu mwa Rais wa China anashikilia nafasi ya pili.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya Temasek Holdings, ya Singapore.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, anashikilia nafasi ya nne.
Wengine ni , mwenyekiti wa kampuni ya PepsiCo ya Marekani. Namba sita ni , Rais wa India. Namba saba imeenda kwa, mtendaji Mkuu wa kampuni ya Anglo American ya Uingereza.
Nafasi ya nane anaishikilia ambaye ni mwenyekiti, kampuni ya Archer Daniels Midland ya marekani.
Namba tisa ni , mwenyekiti kampuni ya Kraft Foods ya Marekani, na namba kumi ni , Mtendaji Mkuu wa Alcatel-Lucent ya Marekani.
anashikilia nafasi ya 21, wakati Malkia Elizabeth anashikilia nafasi ya 23.
Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, , anashikilia nafasi ya 25.
Kama orodha hii ya Forbes inaonesha ukweli na uhalisia wa umaarufu unaotokana na michango ya wanawake katika jamii zao au jamii ya dunia, ina maana kwamba, kwa Afrika, wanawake hawajafanya lolote kwa jamii zao na jamii ya dunia.
Lakini, huo utakuwa pia ni uongo mkubwa, kwa sababu kuna idadi kubwa ya wanawke hapa Afrika ambao wamejitahidi kwa viwango vya kimataifa kubadili hali za watu wengine katika jamii.
Kama ni umaarufu kwa maana ya kujitangaza na kutangazwa sana na vyombo vya habari, ni wazi suala zima linakosa mantiki na linajaribu tu kuwavunja moyo wanawake wa Afrika. Orodha hiyo ni wanawake maarufu duniani katika nyanja za siasa na uchumi, ambapo ni uongo kudai kwamba, kati ya wanawake 100 duniani, Afrika inaambulia nafasi mbili, tena za mwisho.
Hii ina maana dunia inawatambua wanawake wawili tu Afrika katika nyanja hizo? Ndiyo maana naamini kwamba, Migiro angepaswa kuwemo kwenye orodha hiyo, kama kweli inakagua mambo kwa uhalali.
Lakini, mtu akikagua orodha hii tena na tena anaweza kupata picha kubwa zaidi na kuikubali, ingawa baadaye anaweza kuipinga. Ni matokeo ya kura yenye utata. Kwa mfano, Hilary Clinton anafahamika, kama ilivyo kwa Oprah Winfrey, lakini nao wametupwa hadi nafasi za 20, kama ilivyo kwa Malkia Elizabeth.
Lakini, hapohapo kuna majina kati ya namba 11 hadi 20, ambayo ni ya wanawake ambao hata watazamaji, wasomaji na wasikilizaji wazuri wa vyombo vya habari vya nje hawajawahi kuwasikia.
Kama ilivyo kwenye nyanja nyingine, hasa uchumi, vyombo vya habari vya Magharibi, bado vinaitendea Afrika kama vile ni bara wanamoishi wanyama, badala ya binadamu.
Vyombo vyetu vya habari, kwa bahati mbaya, navyo ni kama sauti za vyombo vya habari vya Magharibi.
Vikifanya tafiti zao, vinafanya kwa njia finyu na iliyofubaa, isiyoweza kuwahamasisha Waafrika.
Hii iliandikwa kwenye gazeti la jitambue iliandikwa na Hayati Munga Tehenan.
kwangu mimi mwanamke maarufu ni BIBI yangu....lol
ReplyDeleteKuna wakati huwa sikubaliani na takwimu hizo. Kuna wakati katika watu 50 maarufu wa Afrika Nyerere alikuwa nafasi za chini mno. Mi sikubali kuwa waziri wa Msumbiji ni maarufu kuliko naibu katibu wa UNO.
ReplyDeleteHaya sasa wacha nianze na hii nukuu ya UKWELI WA KWANZA kuwa "Bahati mbaya ni kwamba, kura hizo kwa sehemu kubwa zimehusisha matumizi ya vyombo vya kisasa ambavyo havipo kwa wingi Afrika, hasa mtandano wa intaneti."
ReplyDeleteHili ni tatizo na tatizo hili limeanza kuelekezwa mpaka nyumbani Tanzania ambapo Rais anakusanya maoni na maswali ya waTanzania kwa kutumia simu na email ambazo gharama za kutuma swali ama oni hilo ni zaidi ya wastani wa bajeti ya mTanzania wa kawaida kwa siku. Ndivyo inavyoonekana sasa. Tunaambiwa nani ni mzuri, nani ni maarufu, nani ni rafiki na nani ni adui. Labda kuanzia hapa na viongozi wetu wajifunze kuwa wanapoambiwa mambo wawe wanahoji. Huu ni uthibitisho tosha kuwa "umaarufu" unatokana na MASLAHI YA KISIASA KWA NCHI. Ninapokutana na watu wa hapa huwa wananiuliza kama ninapotoka nami huwa nawatajia TANZANIA. Kisha wanaosema hawaijui nawauliza kama wanaifahamu Rwanda, Burundi, Congo, Sudan, Somalia, Ethiopia, Eritrea, Afrika Kusini na mara nyingi watasema NDIO. Kisha nawauliza nchi kama Lesotho, Swaziland, Botswana na nyingine zenye amani na zisizo na tu-kashfa twa kuchafuliwa hapa watasema hawajui. Nawauliza kwanini wanazijua wazijuazo na si nilizowauliza na mara nyingi jibu ni kuwa ZINAONESHWA WATU WANAVYOPIGANA.
Kumbe kwenye nchi za huku, tukionekana basi si kwa wema.
Na bado wanatupangia la kufanya na WATAWALA WETU wanafuata tuu bila hata kuuliza. Kibaya zaidi WANAIGA MFUMO WAO WA KUJUA NA KUPIGISHA KURA AMBAO UNAWATENGA WENYE UHITAJI HALISI.
Nukuu ya pili ni ile isemayo "Kama ni umaarufu kwa maana ya kujitangaza na kutangazwa sana na vyombo vya habari, ni wazi suala zima linakosa mantiki na linajaribu tu kuwavunja moyo wanawake wa Afrika" Kwa hii naandika kitu kwa jina la "LABDA WANAONEKANA WANA AKILI KWA KUWA HAWANA AKILI" na naamini ntalizungumzia zaidi huko na pengine kuunganisha na makala hii.
Lakini ni wakati ambao tunatakiwa tuamke. Wakati ambao Rais anatakiwa aache kukaa kwenye TV kujibu maswali bali awahimize watendaji wa Kata, Tarafa, Wabunge na wakuu wa mikoa kufanya hivyo angalau kila mwezi ili aendapo huko akutane na shida halisi za mTanzania na sio kupewa maswali na wanaDar-Es-Salaam na wachache walio na uwezo wa kutuma sms.
Ni wakati ambao Rais anatakiwa atulie nchini na kupanga mikakati halisi ya kutumia rasilimali za nchi kuinufaisha nchi badala ya kuendekeza kutembelea nchi za nje kuomba misaada ambayo ikifika walio pembeni yake wanamsaliti kwa kuila. MISAADA HAIWEZI KUWA NA MANUFAA KAMA YATOKA KWENYE NCHI ZINAZOTUANGALIA KWA JICHO LA NAMNA TUIONAYO KWENYE MAKALA HII.
Mengine nitaiongea "NEXT IJAYO"
Blessings
Umewasahau na wale waliotangazwa sana ya kuwa wameuvumbua mlima kilimanjaro, ilhali waliwakuta wachagga wapo hapo miaka na miaka, na yule aliyedai kavumbua ziwa victoria, wakati wenyeji waliokuwepo walikuwa wanaliita ziwa Nyanza.
ReplyDeleteHao jamaa wanajitafutia umaarufu, kuna wengine wanafikiri Afrika ni nchi moja na tena ndogo. Upeo duni kabisa
Mhh!
ReplyDeleteMie chichemi kwakuwa TOPIKI HII SIJUI NIIANZIE WAPI .
...na hata nikianza katika topiki hii kwa kufananisha na ni nini maarufu zaidi kati ya MKOJO na MAVI a.k.a TIMBA,na Ukibanwa na kamasi wakati ni muhimu kupenga,...
..... kushindanisha Mavi na Mkojo KWA UKALI WAKE KATIKA swala zima la HAJA bado kuna mjanja aliita HAJA moja ni kubwa na nyingine NDOGO katika ujuaji wa jinsi avisikiliziavyo akibanwa ,...
...na kwa bahati mbaya bado ukali wa njaa UKIUMWA NA NJAA nafasi ya makali ya njaa utayastukia mkuno wake tu na wakati unausikiliza ukali wa njaa unaweza kuelewa haja kubwa mpaka ubanwe na kiu wakati huna MAJI ndio ustukie kwanini kukojoa muhimu kikojoleo chako kiki kauka.:-(
Samahani unaruhusiwa kutoelewa kuwa tararira yote hii inahusu TOPIKI:
''Mwanamke maarufu kuliko wote DUNIANI'':-(
Si una kumbuka siri ya mwanamke kuitwa mwanamke ni kwa kuwa anauke na kwa hilo haiwezekani mwanamke yoyote anaweza kusifiwa kama mwanamke na KATIKA HILO sio kama andunje wengine duniani kama nukuu haihusianishi umaarufu wa mwanamke bila kunukuu huyo alikuwa na uke?
Tukiachana na kunukuu wenye uume ,.. Si binadamu maarufu kwa kujipendekeza kwa ombaomba India na kusingizia hilo kwa ya kiyesuyesu alijulikana kama Mama Teresa?
Samahani kwa banangenge hii hapa sebuleni kwa Yasinta na Ruksa kutoelewa!:-(
MADA IMETULIA...
ReplyDeleteKITURURU......LOL
Salute kwako kaka Mubelwa, nimependezwa na maoni yako kaka, sina cha kuongeza.
ReplyDeleteKaka Simon Mkodo Kitururu....Mhhh!!
Nawashukuru wote kwa maoni yenu mazuri. Mimi bado najiuliza kwa nini watu wanafikiri kuna mmoja ambaye ni maarufu. Kwa mimi watu wote ni sawa tu. Shukrani kwa wote.
ReplyDeleteDah hongeleni wote kwa mawazo mazuri. Lakini tukumbuke kuwa tusipo jitahidi sisi kama waafrika wenyewe hakuna mzungu au mmagharibi yoyote atakaye tunyanyua, bali kutubeza na hatimaye kutudondosha kabisa. Mfano mzuri ni mama Migiro. Ni mwanamke anayetoka Afrika . Lakin swali ni kwamba sisi kama wa Afrika tumefanya nini kutunza heshima ya mama huyu au tumnasababishia yeye kupoke lawama na mabezo yotu. Kinachotakia na kulekebisha mambo yetu bila kutegema msaada wowote toka nje ya afrika then tutaona kama tutashidwa tena. Yangu ni hayo tu. My name is Kenneth Peter Magunguli from Tanzania.
ReplyDelete