Thursday, December 10, 2009

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA ABRAHAM!!!!!!

Mtoto Abraham miaka 2 leo.


Leo tarehe 10 Desemba 2009 mtoto huyu anatimiza miaka miwili kamili tangu kuzaliwa kwake. Ni furaha iliyoje kwake kushrehekea siku yake hii ya kuzaliwa huku akiendelea kukua kwa umri na kimo pamoja na afya njema.

Safari ya kutimiza mwaka huu wa pili haikuwa rahisi sana kwa mtoto huyu. Mnamo tarehe 20 Juni 2009, binadamu fulani ambao kutokana na tamaa zao za kutafuta fedha kwa njia ambayo ni ya kudhuru, walitaka kukatisha uhai wa mtoto huyu kwa kumtumia kama ngao ya kutaka kupata kile walichotaka.

Akiwa amening’inizwa kichwa chini miguu juu huku panga lenye makali ya kutisha likiwa shingoni, tayari kwa kukata kichwa iwapo wazazi wake wasingetekeleza kile walichotaka wadhalimu hao, mtoto huyu aliendelea kuwa mtulivu.

Wazazi wa mtoto huyu waliona fedha na vitu vingine haviwezi kuwa na thamani zaidi ya ya uhai wa mtoto wao, walikubali kupoteza vyote na sio mtoto wao mpendwa.

Pamoja na msukosuko huo, mtoto huyu ameendelea kukua huku akiwa na afya njema, na furaha tele. Hiyo inadhihirisha kwamba tukio lile ni ishara ya ujasiri alionao.

Mungu amjaalie mtoto huyu akue kwa umri na kimo ili aje aitumikie jamii na kuifanya dunia hii kuwa ni mahali salama pa kuishi.

Happy Birthday Mtoto Abraham Shabani Kaluse.

Picha kwa hisani ya Utambuzi na kujitambua Blog.

9 comments:

  1. Mungu alimjalia mtoto Abraham ili awe jasiri kwa maisha yake yote. Ninamtakia hivyo. Ninamtakia afya njema na maisha marefu.

    ReplyDelete
  2. Napenda kuungana na familia ya rafiki yangu na mwanautambuzi mwenzangu Shabani Kaluse katika kusherehekea siku hii ya mtoto wao Abraham kutimiza miaka miwili leo.

    Tukio lile la kuvamiwa na majambazi, lilikuwa ni la kutisha na la kuhuzunisha pia, kwani lilitishia uhai wao na uhai wa mtoto wao mpendwa.
    Ni jambo la kufurahia kuwa pamoja na tukio hilo mtoto Abraham ameendelea kukua huku akiwa na afya njema na leo anatimiza miaka miwili kamili.
    Namtakia maisha marefu na afya njema na tukio lile liwe ni ishara ya yeye kusimamia amani umoja na mshikamano katika jamii yetu pale atakapokuwa mtu mzima.

    HONGERA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA MTOTO ABRAHAM SHABANI KALUSE.

    ReplyDelete
  3. Abraham 'ongela' kwa siku hii ya kuutafuta ukubwa. ukuwe uje kuwa na akili nyingi mpaka zingine zimwagike chini. uwe injinia au daktari wa watu, au uwe linguist kama mimi.

    ReplyDelete
  4. Nami ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza mtoto Abraham kwa kutimiza miaka miwili kamili leo. Ni furaha iliyoje kwa mama Abraham baba Abraham kwa kusherehekea siku hii ya kuzaliwa ya mtoto wao mpendwa.
    Waswahili walisema yaliyopita si ndwele tugange yajayo…..hii ina maana kuwa tukio lililowapata wazazi wa Abraham kwa kutishiwa uhai wao na wa mtoto wao mpendwa ni mapito lakini yeye Mungu anajua zaidi yetu na labda alikuwa na makusudi yake ili maisha yaendelee, naamini tukio lile linabashiri hekima, ujasiri na imani kwa mtoto Abraham kwani kama jina lake, kwa mujibu wa vitabu vya dini hizi mbili za Ukristo na Uislamu, Abraham anatajwa kama nabii aliyesimamia Amani Duniani na alikuwa na Imani hasa…Tumeona hata kwa Yule Rais Abraham Lincolna wa Marekani na yeye kama Jina lake anatajwa kama Rais aliyesimamia upatikanaji wa haki na usawa kati ya jamii ya Mamarekani weusi na wazungu wa Maraekani.

    HONGERA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA MTOTO ABRAHAM.

    ReplyDelete
  5. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 11, 2009 at 7:53 AM

    Hongera mwanetu eeeeh hongera naye Kaluse aongereeeee....weee hongera!11

    amani na mshikamano

    ReplyDelete
  6. nimeitembelea familia ya Kaluse mara kadhaa na katoto haka kalikataa nikapakate japo mimi sikataliwagi na watoto. natamana kakikua kawe katambuzi na kajitambue ili kasiipende wala kuijua dini kama babake asivyoipenda wala kuijali dini.

    si wanautambuzi hawakasirikagi hata ukiwatukana au kuwadhalilisha, Amina

    ReplyDelete
  7. Kamala watoto wa siku hizi wakitembelewa na mgeni wanategemea zawadi, sasa wewe ndugu yangu ulikuja mikono mitupu, unategemea angekubali kupakatwa na mikono mitupu? LOL
    Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru dada Yasinta kwa kuweka post hii ya kumpongeza mwenetu Abraham kwa siku yake ya kuzaliwa.
    nakumbuka miezi kadhaa iliyopita dada Yasinya aliniomba picha ya mwenetu nikamtumia na baadae aliniuliza kuwa Abraham alizaliwa lini, nikamueleza, lakini sikujua kama dada Yasinta alikuwa na jambo anatarajia kulifanya.
    Siku moja kabla ya kuiweka post hiyo alinitumia email na kuniambia atani suprise, lakini sikumuelewa....
    naomba nikiri kuwa nilisahau kabisa kuandaa zawadi ya kusherehekea siku ya mwenetu kuzaliwa, sijui ni uzembe au ndio nazeeka.
    Ni kweli siku iliyofuata yaani tarehe 10 December 2009, dada Yasinta alinitumia email akinitaka nifungue blog yake kwani kuna kitu....
    Nilipoifungua nilishangaa sana na nilimpigia mama wa mtoto kumkumbusha, kumbe mwenzangu alishaandaa na keki kabisa, na hakuamini kuwa nilisahau siku ya kuzaliwa mwenetu...LOL

    Nawashukuru wote kwa dua zenu njema kwa Abraham.

    ReplyDelete
  8. Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuru wote ambao mmetoa mchango wenu kwa kumpongeza mtoto Abraham. Nami labda niseme machache. Abraham, nakutakia maisha mema, ukue uwe kijana mwenye busara na uwe mtii kwa wazazi wako. Na naamini utakuw hivyo kwani umekwisha onyesha tangu sasa kuwa wewe ni shujaa. Mwenyezi Mungu awe nawe katika maisha yako daima.

    ReplyDelete