Wednesday, December 16, 2009

NGOJA TUANGALIE PICHA ZA LEO!!!!!


Hapa ni Septemba 2009 mwanadada ana manywele ya ajabu kichwani kwake. Na inaonekana kama anafanya kazi ya kublog.

Na hapa ni 16.Desemba 2009 yaani leo Jumatano mwanadada anaonekana ni mwafrika/mTanzania mwanaafro KABISA:-)
Swali je? picha ipi ni bora kuliko nyingine? au tuseme mwanadada awe na nywele za aina gani?

28 comments:

  1. Hiyo picha ya kwanza unaonekana kama upo kwenye jumba la Big Brother..hehehehehe...jamani mnaona eh? na nywele zote zimekupendeza dada...you gotta change sometimes

    ReplyDelete
  2. Mimi bado namuangalia midomo Mwanadada sijafika kwenye nywele !


    Na wakati nafanya hivyo nachofikiria siri yangu !:-(

    ReplyDelete
  3. Picha ya pili, nywele za mwanadada zimenikosha!

    ReplyDelete
  4. dada picha ya kwanza ndio bora, ulipendeza sana na hizo rasta za kimasai, naamini hizo rasta ulisuka huku nyumbani Tanzania...LOL

    Sijui utapata wapi msusi mwingine....au na huko kuna wamasai...LOL

    I love you my Sister....

    ReplyDelete
  5. Mkodo we "kiazi" kwelikweli. Hahahaaaaaaaaaaaaaaaa.
    Comment yangu kwenye hizi picha ni "no comment"
    Asenti

    ReplyDelete
  6. Nimerudi tena, nilisahau kumuuliza Kitururu....
    Kitururu: kaka yangu hebu ngoja kwanza nikunukuu: "Na wakati nafanya hivyo nachofikiria siri yangu !:-(" Mwisho wa kunukuu...
    Sasa hebu nidokeze unachofikiri ni kitu gani hasa kaka yangu?

    Naomba utushirikishe wadau ili tufikiri kwa pamoja maana huenda mwenzetu unafaidi peke yako...LOL

    ReplyDelete
  7. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 17, 2009 at 6:14 AM

    @Yasinta: bado sijapata jibu: twaulizwa picha gani ni bora ama ni nywele gani ni bora....lol

    manake picha na maelezo zinaelekeza tafakuri ya nywele....lol

    ReplyDelete
  8. lazima unatembelea blog ya kufikirisha juu ya siasa kwa mzee wa c/moto au mbelee. ingekuwa ya kitururu ungekuwa unacheka cheka hovyo. si inatekenya ile ehe?

    ReplyDelete
  9. mh! kwakweli mi naona zote ziko bomba ile mbaya.

    ReplyDelete
  10. mwenye macho............
    labda mimi nitazama PUA ilivyo.... ila nami sitasema ninachofikiria

    ReplyDelete
  11. > Kaluse sema unachofikiria kabla hujajua kama unafikiria....Lol....

    ReplyDelete
  12. Nilikuwa naangalia gharama za kusafiri kuja kutembea Sweden..Mhhhhhhh

    ReplyDelete
  13. Zote ni bomba ile mbaya, labda kata nywele ili tuzidi kulinganisha..

    ReplyDelete
  14. hakuna hata moja uliyopendeza hapo. labda jaribu kunyoa nywele zote (zungu)

    ReplyDelete
  15. SAMAHANI KWA MNURURISHO UFUATAO;
    dada Mija anasema kunyoa nywele, halafu kuna asiyejulikana huyo anasema kunyoa zungu...duh! nilidhani kunyoa afrikia???/ aaaah ok. kumbe ile kunyoa TAKO?

    ReplyDelete
  16. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 17, 2009 at 2:23 PM

    moja ilipigwa wakati ametia mekapu na nyingine akiwa nachuro (nadhani alikuwa ametoka kuoga)....lol


    sasa ipi nzuri ya mekapu ama ya nachuro?....lol

    ReplyDelete
  17. Picha nzuri ni ile ambayo unapigwa punde unapokurupushwa. Yaani kabla hujajua kuwa mpigaji ana kamera.
    Ama ile itakayokutaimu wakati unapiga chafya. Hizi mbili ndio hasa zinazoonesha UASILI wako maana katika haya huwezi kujibadili.
    Kama unayo ya hivyo ongeza hapa tuweze kufananisha zaidi.
    Nadhani ntapenda utakayokuwa unapiga chafya.
    Just trying to be optimistic

    ReplyDelete
  18. picha zote mbili ni bomba sana dadangu, ila inategemea jicho la mtazamaji ameegemea upande gani kwa wale wanaopenda vitu halisi ni wazi ataikubali ya pili kuliko ile ya kwanza ambayo inanwyele bandia na ambazo huwazingua wengi kwani kipya kinyemi,binafsi napenda sana kitu halisi.

    ReplyDelete
  19. Asanteni wote kwa kuzipenda hizo taswira. Kusema kweli kupata msusi huku ni kasheshe sana ndio maana huwa nakaa na minywele muda mrefu ni kweli nilisuka nyumbani Tanzania. Labda nifuate ushauri wa Chacha na Da mija ninyoe kama Flaviana Matata....LOL. Shukrani woooooooote.

    ReplyDelete
  20. tunapo zungumzia nywele tuzungumze nywele tu natukizungumza kamba au nyuzi tutambuie baina ya nywele na nyuzi huwezi kufananisha nywele ni necture yani zime tulia

    ReplyDelete
  21. my response y8g93j8p38 replica louis vuitton bag replica bags aaa a8x84h6j42 replica bags on amazon hermes fake c0y81y6k27 replica bags online replica goyard bags replica gucci bags u8z05m3r69 zeal replica bags

    ReplyDelete