Tuesday, December 15, 2009

Kamala Lutatinisibwa:- nawowa jamani nafunga ndoaz

Kamala Lutatinisibwa,
kuna mijadala miingi kuhusu ndoa, kufunga ndoa na harusi katika jamii yetu. kwakuwa naishi katika jamii, nimejikuta nami nikipaswa kufunga ndoa ya kanisani kwani kumbuka kanisa sio baya na nizuri.

basi weekend hii jpili saa 7 mchana, mimi na my beloved waifu tutavaa nguo mpya na kwenda mbele ya hadhira na pasta ili tuvalishwe pete na kukla viapa kidogo nakiasi katika kanisa la KKKT pale posta.

wanablogu woote mnakaribishwa. kutakuwepo na kijisheree kidogo tu na hakuna mchango wala nini kwa wanaojisikia njooni tu.

tumelazimika kufanya hivyo baada ya wife kupata kazi anayoipenda katika KKKt na hivyo hawezi kuajiriwa nakuzaa bila kufunga ndoa kwani itakuwa muujiza huo.

NB; Chacha Wambura ndiye atakuwa bodyguard wangu siku hiyo

20 comments:

  1. Hongereni sana hii ni hatua muhimu katika maisha

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Kaka hilo ni wazo zuri ktk maisha ya mwana damu mungu hawa tangulieni

    ReplyDelete
  3. Kwa mara nyingine Hongera Komandoo Kamala! Kwenye blogu yako ulivyobobea kwenye mada za ndoa nilianza kuhisi ndoa inanukia.

    DUH yani Mkuu wiki ijayo ndio utakuwa hufanyi tena matusi mpaka ufe kama utafuata maadili Kanisa lililotunga. Na inasemekana wafanya matusi wakianza kufanya tendo la ndoa , hamu na jaziba ya kulirudia tendo mara kwa mara hupungua.:-(

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Kamala. Lakini.... kama asingepata hiyo kazi, basi mweee mweee

    ReplyDelete
  5. Ni wazo zuri kaka kuamua kuachana na uasherati, maana ukishaoa inabidi uvae lipete likuubwa ili kuwatisha wakuda wanaozengea wanaume za watu kwa kutaka kuwachuna......LOL

    Sijui ndoa inafungiwa kanisa gani maana naweza kuja....LOL

    ReplyDelete
  6. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 16, 2009 at 5:23 AM

    @Mkuu Kitururu: ni hamu ama mshawasha....lol Duh ;>)

    @Koero: hao wakuda wako wapi mbona musoma siwaoni...lol japo nipo nipo sana lakini ninalipete likuuuubwa.....lol

    kuhusu kanisa ni "kanisa la KKKT AZANIA FRONT pale posta".

    Ntakuwepo hivo ukija unaweza kupata EMCHEKU....lol

    ReplyDelete
  7. Ndugu yangu Chacha oWambura Ng'wanambiti Mtambuka Malogo kuhusu emcheku, nadhani umechelewa kwani nilishapigiwa zamaaani na sasa jamaa anamiliki mali zake....LOL

    Pamoja na kwamba upo upo kkwa sana lakini ukija usivue hilo lipete lako maana usije ukajikuta umehamia Dar na kusahau Musoma.
    Kaka jiji la DAR ni la Moto, huku utakutana na Vi mini na suruali mlegezo, utahimili vishindo wewe na ushamba wako wa Musoma?

    Kaaaaazi kweli kweli....Welcome to DAR ES SALAAAM Ng'wanambiti.....LOL

    ReplyDelete
  8. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 16, 2009 at 6:42 AM

    @Koero: nkipata wa kunitunza si mbaya saana..lol

    zamani nakumbuka kuwa kulikuwa na mijadala ya shuga-dadi sasa nasikia mijadala ya shuga-mami vs serengeti boys....sasa nami nataka kuwa serengeti boy ;>) kuna kijana nilimkodi toka hotel moja hapo Dar wiki ilopita anipeleke eapoti akanambia kuwa ana mke na watoto lakini kuna JIMAMA jitu zima tu lime-EMCHEKU na kumnnunulia hiyo gari kwa mkopo ambapo anapaswa kurudisha sh 40,000/= kwa mwezi lakini kila wiki lazima 'amege tonge' mara mbili na hivo ratiba yake ni nyumbani 'mara 2' na kwa jimama mara mbili....lol

    umenambia ya dar na kwa kuchanganya na hili..duh! nshakuwa mwoga kama mseminari anayetaka kuwa padre ilihali anataka kumega tonge la....lol

    ni vijimambo tu... ;>)

    ReplyDelete
  9. Chacha oWambura....Duh,
    Kama ikipita siku moja Dar ni kama mwezi, yaani kuna mabadiliko kila sekunde, kwani hiyo tangu uongee na reva Tax hesabu imepita miaka sita, unajua kilichompata huyo Dereva Taxi?
    Kaolewa yeye sasa....LOL

    Ndugu yangu Huku Dar kaka Vibinti wanaongoza kwa Kuwa emcheku wanaume badala ya wao kupigiwa emcheku, na hata huyo Kamala usishangae kusikia kuwa ni yeye aliyepigiwa emcheku......LOL

    Kamala: Nyoooo....Hivi kweli wewe ndio wa kusubiri mpaka kufunga ndoa ndio uonje.....LOL
    Hebu kuwa mkweli wa nafsi yako...tuongee pembeni watu wasisiskie....(Hivi kweli hujaonja kaka?)
    Kwa jinsi ninavyowafahamu wanaume thubutuuuu....asubiri ridhaa ya Kasisi au Shehe...Kalagabaho...

    Tatizo ni kwamba, wanaume mmezidi udadisi mno, mtapekua weee mpaka mtoweze.....LOL

    Kitururu hivi Matusi ni nini vileee!!!?????

    ReplyDelete
  10. hongera Mwenyekiti Kamala wasaaalam hapo uliPo salaaaaaaam tele kwa shemeji RICHACHA WAMBURA RENYEWE ITABIDI RIFANYE KAZI YAKE IPASAVYO!

    ReplyDelete
  11. KUONJA MUHIMU KAKA USIJE UKAUZIWA KABABU KWENYE GUNIA WAKATI UMEAGIZA PIZZA.

    Ndiyo maana najiuliza kama kosa lilikuwa la ADAM NA EVA kama wanavyotusadikidikisha... sasa ya nini tubambikiziwe wengine kwa EMCHEKU ya hawa jamaa???????????????????????????????????
    kwanza ndoa NI NINI? SITAKI JIBU LA KUZAA WATOTO NA KUISHI WAWILI...KWANI HATUWEZI KUISHI WAWILI KATIKA DUNIA YA AINA MOJA??? DUH NA KUJAMBA TUJAMBE WAWILI....LOL..........

    ReplyDelete
  12. Kwani Kamala na Koero mmemaliza? Looooooooooooool. SIMO
    Anyway, najua Kamala uko busy KUKARIRI sala ya bwana na mengine mengi ili usije umbuka. Ila ni OPEN BOOK kwa hiyo usijali.
    Nasubiri kuendelea kusoma "maoni" yako na Koero.
    Lol

    ReplyDelete
  13. @Komandoo Kamala: Mheshimiwa ulishafanya maombi Mamaa asiwe mwezini siku ya mambo yote RUKSA?

    Kwa maana nasikia ni nuksi katika NDOA kupata mfadhaiko kisa hali halisi Bwana harusi imebidi anyimwe tunda la ufahamu kwa kuwa mida mida bado ni tunda damu usiku wa ndoa.

    :-(

    ReplyDelete
  14. @Kadinali Ng'wambiti: Ni hamu na Mshawasha.:-)

    @Koero: Nanukuu ``Kitururu hivi Matusi ni nini vileee!!!?????´´ mwisho wa nukuu.


    Ngojea nitafute Kamusi ntakujibu.

    ReplyDelete
  15. Una kuvutia sana blog.
    Salamu kutoka kwa ubunifu na ubunifu photos ya Jose Ramon

    ReplyDelete
  16. Hongera sana Kamala karibu kwenye chama chetu

    ReplyDelete
  17. Nami ngoja niseme nadhani sijachelewa HONGERA SANA Kamala.

    ReplyDelete