Friday, December 25, 2009

MSAADA.....Namtafuta RENATHA BENEDICTO

Heshima kwako Ndugu.
Naomba uniwakilishie ombi hili barazani kwako. Namtafuta Dada Mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 7 sasa.
Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu.
Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako
http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html )

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka uliofuata na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio.
Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.
Email yangu ni changamoto@gmail.com

5 comments:

  1. Nawatakia Krismas njema.
    Natumaini na Mubelwa atafanikiwa kumpata ndugu yake

    ReplyDelete
  2. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 26, 2009 at 10:05 AM

    Natumai utampata tu kaka

    ReplyDelete
  3. Sijui kwanini naanza kufikiria Dada Renatha anasifa zote za kuchumbiwa!

    ReplyDelete
  4. Mubelwa usikate tamaa utampata tu Da Renatha nina kaushauri je huwezi kuweka tangazo kwenye Rrdio maria pia? ni wazo tu maana mtu inabidi ujaribu kila njia.

    ReplyDelete