Hii nimeipata katika Jamii forum nimeona niiweka hapa ili nanyi wasomaji mcheke kama nilivyocheka mimi, karibuni.
Kulikuwa na jamaa watatu kila mmoja alitoa sifa yake ya kufanana na mtu maarufu duniani.
Wa 1, mimi wananifananisha na Idd Amini
Kwa sababu gani?
Kutokana na umbile langu refu na rangi yangu nyeusi watu wananifananisha na Marehemu Idd Amini dada.
Wa pili: Mimi na Osama bin Laden
Kwa sababu gani?
Kutokana na weupe wangu na ndevu nyingi hata jina langu limekufa siku hizi naitwa Osama
Wa tatu ambaye alikuwa na umbile dogo kuliko wote.
Mimi nafanishwa na Mungu
Watu wote walishtuka na kumuona yule jamaa kama anamkufuru Mungu lakini aliwathibitishia kweli kuna mtu alimfananisha na Mungu.
Najua hamuwezi kuamini kama mjuavyo mimi mwenzenu mpenda ulabu na vifungu haviniishi, kila nilipopelekwa polisi nilihukumiwa na hakimu mmoja siku moja baada ya kupanda kizimbani hakunihukumu bali alinieleza kuwa ameniachia huru na nisirudie kufanya tena makosa.
Lakini kwa bahati mbaya nilikamatwa na kupandishwa kizimbani, na hakimu alikuwa yule yule wakati napanda alikuwa ameinama akiandika ripoti baada ya kuandika aliponyanyua macho akaniona na kushtuka huku akisema.
Mungu wangu umerudi tena
Bado tu hamjaamini kuwa niliitwa Mungu, jamaa alibakia wakitazama kutokana na mwenzao kushindwa kumuelewa hakimu alikuwa na maana gani na si kumfananisha na Mungu
hii kali ya kufungia mwaka
ReplyDeleteNami nimeikubali ni kali ya kufungia mwaka.
ReplyDeleteDunia hii kwa visa!!!...
ReplyDeleteteh! teh! teh!
ReplyDeletedah :-0
du mimi Markus a.k.a MCHARUKO nafanana na PAKASHUME
ReplyDeletekaka Bennet! ni kweli.
ReplyDeleteMtani Fadhy! sawa kabisa.
Da Mija! nakubalina nawe Dunia hii ina visa tena vya hali ya juu
Ng´wanambiti! teh! Teh! teh!:-)
Markua afadhali wewe unafanana na PAKACHUME. Mie nafanana na mimi:-)