Nawaza ni mwaka 2011 na nipo pale Ikulu, Rais Rev. Kishoka, natafakari cha kufanya ili kusisimua uzalishaji wa ndani na naita mkutano na Wafanyabiashara kupitia TCCIA, Wizara ya Biashara, Chama cha Wakulima TFA, Wizara ya kilimo, uvuvi na mifugo na watu wa TBS, Chakula Bora na Waziri Mkuu.
Tukiwa tunakunywa maji ya matunda ya Maaza na kufinyanga vipande vya nyama vilivyonunuliwa shoprite na mkusanyiko huo kuhudumiwa na Movenpick, nawauliza wote walioko,
"je ni lini nitaweza kutumia kila kitu pale Ikulu na hata kununua madukani bidhaa zinazosema "made in Tanzania"?
Wakiwa bado wanatafakari, nitawarushia kombora jipya na kutoa amri ya upole kuwa ikifika mwaka 2013, nataka nione kuwa kila kona kuna bidhaa zilizotengenezwa Tanzania na kuzalishwa Tanzania! Zaidi natoa amri kwa mtu wa Ikulu, Luhanjo wangu kuwa kuanzia siku hiyo, ni marufuku kwa Ikulu kutumia bidhaa kutoka nje, ikiwa bidhaa hizo zinazalishwa Tanzania na tunauwezo wa kuzitengeneza (manufacture) zitumike.
Nitawageukia Wafanyabiashara, Wakulima na Mawaziri wa wizara husika na kuwauliza, wanahitaji nini kutoka kwangu na Serikali yangu ili mkate, siagi, maziwa, matunda, asali, chai, soda, bia, mvinyo, mayai, nyama, mchele, mahindi na aina yeyote ya Chakula kinachopikwa na kutumika Ikulu ni mali ya Tanzania kutoka kwa Mkulima wa Kitanzania na kusindikwa kwa ubora wa kimataifa na kampuni ya Kitanzania?
Nitaendelea na kuwauliza Wafanyabiashara wenye viwanda, ni lini Ikulu itaanza kutumia karatasi zinazozalishwa Tanzania kwa kutumia miti ya Tanzania? ni lini penseli, kalamu na samani za ofisini na nyumba za Ikulu zitakuwa zote ni mali ya Tanzania kuanzia malighafi mpaka zao la mwisho?
Je itakuwa ni makosa kutoa amri na agizo kama hilo na kuwataka wanieleze wanataka nini kutoka kwangu ili mimi kama Rais wa Tanzania na Raia wa Tanzania waanze kujivunia matunda ya mazao yetu na si kufikiria mara mbili mbili tukienda Shoprite ambako asilimia 97% ya bidhaa ni kutoka nje ya nchi?
Hivi kutakuwa na ubaya gani ikiwa VOIL na Tanbond ikawa ndio chaguo la Mtanzania badala ya Blue Band na Korie?
Je ni dhambi kuona kuwa nyama na vyakula vinazalishwa Tanzania kwa ubora kama ule wa zile nyama za Farmers Choice kutoka kenya au zile nyama za Afrika Kusini?
Je ni dhambi kuona kuwa tunaanza kutengeneza samani nzuri kwa kutumia mafundi wetu na viwanda vyetu badala ya kuagiza kutoka Dubai?
Je nitakuwa nimekosea kutoa hamasisho kama hilo kwa Wafanyabiashara ili kuzindua upya shughuli za Uzalishaji mali wa nchi yetu kitu ambacho kitatoa ubora wa bidhaa zetu na zaidi kutoa ajira kwa Watanzania na kuachana na uagizaji wa bidhaa na vyakula ambavyo tuna uwezo mkubwa wa kuzalisha wenyewe na hivyo tuache kuomba mikopo au kutumia fedha zetu za kigeni kununulia vitu ambavyo tunavyo hapa hapa nchini?
Mada hii iliyoandikwa na Rev. Kishoka kwenye Jamiiforum nimeipenda na nikaona ni vema niiweke hapa ili wengi tuione na kusoma.
dada hata Nyanya, apple, biringanya, vitunguu nk, vinatoka South africa, sijui mkulima wa kule Lushoto au wa pale Kihesa Iringa na yeye akuze wapi bidhaa zake. Nimekuwa nikijiuliza kama kosa ni la kwetu wenyewe kwa kutozalisha mazao yenye ubora au ni la serikali kwa kutotoa elimu kwa wakulima wadogo wadogo mbinu za kilimo cha kisasa. bado najiuliza
ReplyDeletekaaaaaaaaaaaazi kweli kweli
ReplyDeleteKazi siyo kidogo. Ingekuwa hivyo mbona raha! Viongozi wangekuwa na dhamira hiyo tungepiga hatua sana.
ReplyDeleteDhamira inaanzia kwako wewe msomaji wa habari hii
ReplyDeleteKaka Shabani ni kweli inasikitisha sana kuona waTanzania wanapenda sana vitu vya kutoka nje. Tuchukue mfano wa nguo mtu anaacha kununua kitenge na kuchona nataka nguo zitokazo ughabuni kwa vile tu zinatoka ughaibuni. Anaacha utamaduni wake kabisaaa hii inauma sana.
ReplyDeleteSimon ni kweli kazi kwelikweli tena kubwa tu.
Fadhy ni kweli tungepiga hatua kubwa sana. Sijui nagombee angalao hata ubunge...lol.
Chib! umenene. Shukrani kwa wote.