Monday, November 30, 2009

NYIMBO ZA MCHAKAMCHAKA/KUMBUKUMBU

Leo nimekumbuka wakati nasoma shule hasa shule ya msingi saa kumi na moja alfajiri kuwahi shule kisa nini? Kuwahi namba na kukimbia mchakamchaka huku mnatweta kama nini na mkiimba nyimbo:- Kwa mfano:-
1. Panda mlima panda, panda, panda, pasnda usichoke........x2
2. Iddi amin akifa mimi siwezi kulia nitamtupa kagera awe chakula cha mamba.x2
3.Jua lille literemke mama, mwezi nao uteremke mama haiyahiyaaa hiyaa hiyaa mamaaaa.....x2
4. Alisema, alisema, alisemaaa Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea shart tuanze mchakamchakax2.....

Kama kun mtu anakumbuka wimbo mwingine basi karibu kuongezea hapa.

23 comments:

  1. hpa ndo huwa nakufaga na hasa nikitembelea vibada (shule) au madarasa tuliyosomea enzi zetu mnakimbia mchaka mchaka harafu darasani mpaka jioni bila kuoga wala nini

    ReplyDelete
  2. Da Yasinta umenipa raha. Nilikuwa nikipenda mchakamchaka hakuna tena. Leo niwaonapo watoto wa shule wakiwa goigoi husikitika sana. Mchakamchaka ulitufanya kuwa na miili imara na akili zenye kuchemka. Najua kuna watu hawakuupenda ndo maana huwa wanauponda.
    Pia nyimbo zake zilikuwa ni zenye kueneza sera fulani.
    Umenifurahisha sana leo.

    ReplyDelete
  3. mchaka mchaka ulikuwa safi sana.Kwanza mwanafunzi inamsaidia mwili kuwa katika hali nzuri.

    ilikuwa safi sana

    ReplyDelete
  4. Hivi kwani siku hizi hakuna mchakamchaka? nimepitwa na habari hizi. Ulikuwa safi sana ni kweli alivyosema Mr Edwin apo juu. kwakweli Mlongo unatukumbusha mbali sana nimejikuta naanza kuimba na kukumbuka ennzi za shule na kale kabaridi ka lilambo ilikuwa inatusaidia kupata kajoto kabla ya kuingia dalasani.

    ReplyDelete
  5. Kuna mengi ya kukumbushana enzi zetu za CHANDIMU na michezo ya kiBabaBaba na Kombolela naa.....

    ReplyDelete
  6. Siku hizi kwa kweli sio mchaka mchaka tu bali hata michezo mingi kama kidali, kibaba baba, mdako, kombolela/butua
    Watoto wako busy na video games hawajui hata kutengeneza magari ya makoa au midoli ya kufinyanaga na udongo, mipra ya chandimu na mengineyo, hii ni kwa sababu ya mabadiliko au maendeleo ya nchi

    ReplyDelete
  7. Weeeee Nampangala ndiyo nani?????? jieleze kwa jina lako hilo harakaaaaaaa.


    Mmmmh dada Lelu unihokonywili kweliiiiiiii, mwenga kotokunihokonyola nahaa wenga, raha weeeee

    ReplyDelete
  8. 1. Bandaa wa Malawi.. katuvalia ngozi ya simba.. kututishia watanzaniaa, hatujali hatujali..

    Mchaka-mchaka chinja, alinselema alija...

    ReplyDelete
  9. Jamani mambo haya.......
    kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  10. @ yasinta ... umoja wimbo/ uwingi nyimbo.

    nilikuwa nasubiri nani ataukumbuka 'mchaka, mchaka chinja, alinselema alija'. nimejua hivi karibuni kuwa wimbo huu wengi tulikuwa tukiukosea. ni wa asili ya kisukuma ndio maana Mija kaupatia. unatokana na mapigo ya waendesha mitumbwi. uwongo? sie tulikuwa tukiimba 'alinselema adija'

    mwe!

    ReplyDelete
  11. 'mchaka, mchaka chinja, alinselema adija'...hapo umeniacha hoi-nakumbuka sana.

    Kwakweli warejeshe mchaka mchaka,lakini sio kuleta tena ile dizaini ya kumalizia kila kitu na"kidumu chama cha mapinduzi".

    P.s. kuna mwimbo mwingine wavita vya Kagera/ nduli Idd Amin ambao nimeusahau.Ulikua unaanza na "lile,lile lilelee"halafu katika unaingizia kwamba alitaka kuiba Kagera "ambayo ndio mali ya Watanzania"...sijui kuna anayeukumbuka?

    ReplyDelete
  12. Lile lile lilembeee,...x3 lile lile lile lilembe, ni mshenzi sana Aminii.., kafikiria sana kashindwaa.. kaona achukue Kageraa ambayo ni mali ya watanzaniaa...

    *Anony hapo juu wimbo huo, mi inabidi tufanye utaratibu wa kuzirekodi ili historia isipotee, hebu ona tunavyohangaika kuzikumbuka.

    ReplyDelete
  13. mija tunakupa shuguli hii rasmi. nina uhakika imetua katika mikono salama.

    ReplyDelete
  14. teh teh teh....abana daah! umenikumbusha mbali kweli kweli huku na ufagio mkononi... ha ha ha. ahsante mama,,,,

    ReplyDelete
  15. Nyimbo number 3..ilikuwa mara yangu ya kwanza kuchelewa shule na ya mwisho! maana dah...

    ReplyDelete
  16. Mwaipopo shughuli ipi unayonipa ndugu yangu?

    ReplyDelete
  17. "mi inabidi tufanye utaratibu wa kuzirekodi ili historia isipotee"

    mija hapo vipi?

    ReplyDelete
  18. Nilitaka kuandika ... mi naona inabidi tufanye utaratibu wa kuzirekodi, Mwaipopo unaonaje tukamwomba Jide aokoe jahazi?

    ReplyDelete
  19. kwani mija mambo ya sanaa siku hizi umeyaweka kando? au wewe kuimba si kihiiiivyo. Lakini nadhani tumifika pahala pazuri. ushauri wa ufundi tutachukua kwako. kuhusu nani aimbe pemgine ni vema tukawamobile watoto fulani hivi (mfano wa vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu) ili sauti hasa siwe za kitoto/watoto. hapa sidhani tutakosa msaada kutoka wizara za elimu, habari na maliasili. au?

    ReplyDelete
  20. Nimekukubali Mwaipopo. Nitalifuatilia suala hili.

    ReplyDelete
  21. Ni furaha ilioje kuna wengi mmefurahia kukumbuka enzi zile na nyimbo za mchaka mchaka. Na nimefurahi kusoma ya kuwa mnataka kufanya mikakati na kuzirekodi hizi nyimbo ili ziwe kumbukumbu zaidi kwa wajukuu wetu. Mie nipo tayari kuziimba..lol. Ahsanteni sana kwa maoni yenu.

    ReplyDelete
  22. Imagine leo ndo nimeona comments. Mchakamchaka ilikuwa raha sana

    ReplyDelete