Ni furaha kubwa kuweza kuchukua nafasi hii, na kushukuru jambo lolote zuri/jema na pia kuzikubali changamoto zinazotolewa. Leo ningependa kuwashukuruni wote kwa maoni yenu mazuri. Kwa kutembelea blog hii , kweli nasema upendo wenu na mshikamano ni mafanikio makubwa kwa mimi na pia kwenu. Kwani kama wote tujuavyo blog bila maoni hatuwezi kujua mafanikio na mapungufu yake. Kwa hiyo kwa jambo hili napenda KUWASHUKURUNI WOTE, NA NASEMA PAMOJA DAIMA bila kusahahu UPENDO DAIMA!!!!!
Da Yasinta, tunashukuru sana kwa kutushukuru kwako. Maisha ya kublog ni ya ajabu sana. Nilipoingia katika ulimwengu wa kublog, nimejifunza mambo mengi sana. Ni ulimwengu wa kipekee utoao uhuru wa kueleza fikra zako na kutoa uhuru wa majadiliano juu ya fikra hizo. Mi nasema kublog ndiyo nyenzo sahihi ya mawasiliano.
ReplyDeleteHivyo hukuza urafiki miongoni mwetu. Huchochea kuwajibika. Hivyo ni jambo la kawaida kila wasaa unajikuta una deni kwa marafiki/wasomaji wako. Kila mara unafikiria uwajuze kwa lipi.
Kwa mantiki hiyo, kublog kunaongeza sana uwezo wa kufikiria na uelewa wa mambo. Kublog kunakuza roho ya kujitolea. Mtu anafanya utafiti na kisha anautoa blogini pasipo kipato chochote. Ni jambo lenye kujenga mahusiano yenye thamani.
Nimesema mengi, la muhimu ni kukushukuru sana wewe kwa kuingia katika ulimwengu wa kublog.
umnikumbusha ki-YCS-YCS vile....lol
ReplyDeleteThanxx dada Yasinta ,Ubarikiwe sana ....Stay showered with blessingz....Cheerz
ReplyDeletekublogu kama aina fulani ya bangi hivi.
ReplyDeleteMwaipopo.... DUH!!!
ReplyDeleteTunashukuru Da Yasinta kwa kutujali, japo wengine ndio hivyo tena tunapitia mara chache
ReplyDeleteSijui nani kati yangu na wewe anapaswa kumshukuru mwenzake. Lakini ntapokea shukrani hiyo nikikushukuru kwa kufanya kile ambacho kimenifanya unishukuru.
ReplyDeletePamoJAH
Lovely Iris's did some nice young man give them to you? I hope so.
ReplyDeleteahsanteni wote. Na mnapendwa wote Upendo daima.
ReplyDelete