Kaka Laurent Kinunda.
Katika ukuaji wangu/akili yangu nilikuwa nafikiri ya kwamba ndugu ni yule mliyezaliwa mama mmoja na baba mmoja. Lakini kumbe nilikuwa na mawazo finyu. Ndugu ni mtu yeyote yule sio TU yule mliozaliwa tumbo moja.
Ilikuwa mwaka 1993 nilipokutana kwa mara ya kwanza na kaka LAURENT KINUNDA. Kaka Laurent, napenda kukushukuru kwa moyo ulio nao, wema wako na upendo wako. Umekuwa karibu sana nasi. Umekuwa huna kinyongo na familia yangu mara kunapotokea shida pia kunapokuwa na raha unakuwa nasi.
Nakumbuka kila tujapo TZ, hakuna mwingine anayekuja kutulaki uwanja wa ndege, isipokuwa ni wewe kaka Kinunda. Kwa hili napenda kutoa shukrani zangu/zetu za dhati. Umekuwa nasi katika matukio mbalimbali na umetusaidia na unatusaidia mambo mengi ambayo siwezi kuyahesabu hapa. Ninachoweza kusema. NAOMBA MWENYEZI MUNGU AKULINDE WEWE NA FAMILIA YAKO MUWE NA AFYA NJEMA NA MAISHA MEMA. TUNAWAPENDA WOTE. UPENDO DAIMA.

mola atambariki na kumwongeza mara dufu, nawe kwa shukrani za dhati "ubarikiwe sana".
ReplyDeleteamen
ReplyDeleteMjukuu wako anasema hivi: 'ni watu wachache wanaoweza kukumbuka fadhila na kutoa shukrani'. hivo nawe twakushukuru kwa kuwa na moyo wa shukrani.
ReplyDeleteBiblia yasema 'ubariki nawe utabarikiwa' sikumbuki ni fungu la ngapi labda Mt saaaana Simon aweza kutukumbushia...lol
Mjukuu wako anasema hivi: 'ni watu wachache wanaoweza kukumbuka fadhila na kutoa shukrani'. hivo nawe twakushukuru kwa kuwa na moyo wa shukrani.
ReplyDeleteBiblia yasema 'ubariki nawe utabarikiwa' sikumbuki ni fungu la ngapi labda Mt saaaana Simon aweza kutukumbushia...lol
mora ambariki...
ReplyDeleteKama alivyosema "Ng'wanambiti" - ni watu wachache wakumbukao fadhila walizotendewa. Wengi husahau fadhila mapema na kuanza kulalamika na kulaumu unapowasitishia misaada. Asante kwa moyo huu.
ReplyDeleteChacha - mbona unajiita Ng'wanambiti?
blessed is the hand that giveth, not the one that taketh.
ReplyDeleteMatondo, hilo ni jina nililopewa wakati nakwenda kwenye ngoma za 'manyalali'...lol
ReplyDeleteNa kweli sio wote wanakumbuka fadhila,na wewe ni wapekee ubarikiwe sana.
ReplyDeleteDada Yasinta, naungana na wadau wanaosema unafanya vizuri kukumbuka fadhila. Halafu, hao akina Kinunda asili yao ni kwetu Litembo, kule juu milimani Umatengoni. Basi leo umenifanya nitembee kifua kijuu :-)
ReplyDeleteNachukua nafasi hii kwa kuwashukuru wote kwa kumsalimia kakangu wa hiari. Kaka Kinunda Ubarikiwe sana na Mungu na uendelee kuwa na Moyo huo huo ulio nao ikibidi zidisha. Sisi hatutakusahau milele.
ReplyDelete