Wednesday, November 11, 2009

POLE KWA MSIBA DA MDOGO KOERO MKUNDI

Nimetoka kazini nimerudi nyumbani, baada ya muda nafungua computer na nasoma ujumbe wenye kicha cha habari NIMEFIWA kutoka kwa da mdogo Koero Mkundi usemao hivi:-
DADA KUNA MAPOROMOKO YA MLIMA YAMETOKEA HUKO UPARENI KIJIJINI KWA MAMA YETU NA KUNA WATU ZAIDI YA 20 WAMEPOTEZA MAISHA MIONGONI MWAO KUNA NDUGU ZAKE MAMA YAANI SHANGAZI YAKE NA WATOTO WAO NA MJOMBA PIA WAMEKUFA, HIVYO KESHO NASAFIRI NA MAMA KWENDA UPARENI KUHANI KWANI WAMEZIKWA LEO HII...... WOTE TUKO HAPA NYUMBANI TUNAOMBOLEZA...........ILA BIBI KOERO NI MZIMA TEGEMEO LANGU. Habari zaidi soma hapa.

12 comments:

  1. Pole sana Koero.
    Yasinta yatinikulonda muda wungi! nivili nilyunga chidogo.

    ReplyDelete
  2. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!November 12, 2009 at 8:46 AM

    Pole sana Da Koero. Mungu akupeni shime muweze kuuchukua msiba huo kwa matumaini makubwa.

    ReplyDelete
  3. pole sana na uwe mwenye uvumilivu na sala katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  4. pole sana da Koero. Mungu akupeni faraja ktk kipindi hiki kigumu kwenu. Pia roho za marehemu zipate pumziko la amani milele. Amina.

    ReplyDelete
  5. aliumba milima na mabonde,
    akaumba vitu na viumbe,
    akawapa sekunde,
    siku ikijiri,aende kwake,
    mtindo wake,mauti yake
    ajali,maradhi yake,
    volkano, au malale,
    mola ajuaye siku yake

    Polani anamwali,
    Osalile pa mbili
    nchito ya Nnungu
    afuna iye kwatu,

    MUNGU AW NANYI

    ReplyDelete
  6. Mwenyezi Mungu nakuomba awalinde Koero na familia yake wasafiri salama. Bikira Maria mama wa Mungu nawe watazame watu hawa na uwape nguvu na utulivu. Amina.

    Poleni sana. Marehemu wote wapumzike kwa amani, amina.

    ReplyDelete
  7. Pole sana Dada Koero pamoja na wanandugu wote, Mungu awape ujasiri na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  8. Pole sana KEORO na huu ni msiba wa Taifa maana unatuhusu wote.Nasikia hizi mvua ndio zinaanza nazinategemewa kubwa kwa hiyo tujihadhari sana

    ReplyDelete
  9. Naungana na Wenzangu kumpa pole Dada Koero na familia yake!

    ReplyDelete
  10. Kweli naamini ya kwamba kublog si kublog tu bali pia kumetufanya tuwe familia moja na napenda sana jinsi tunavyoshirikiana kwa shida na pia raha. Mungu awabariki wote.

    ReplyDelete