Thursday, October 22, 2009

NGOJA LEO TUANGALIE BAADHI YA METHALI ZETU KUANZIA A MPAKA Z

  1. A. Akili ni nywele, kila mtu ana zake.
    Asiyefunza na mamaye, hufunzwa na Ulimwengu.
  2. B. Baada ya dhiki, faraja.
    Bendera hufuata upepo.
  3. C. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
    Cheruru – Si ndo! Ndo! Ndo!.
  4. D. Damu nzito kuliko maji.
    Dawa ya moto ni moto.
  5. F. Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu hulingámua.
    Fimbo iliyo mkononi, ndiyo iuayo nyoka.
  6. G. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
    Gonga gogo usikilize mlio wake.
  7. H. Hapana siri ya watu wawili.
    Heri kujikwaa dole kuliko kujikwaa ulimi.
  8. I. Ikiwa hujui kufa tazama kaburi
    Iliyopita si ndwele, ganga ijayo.
  9. J. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
    Jungu kuu halikosi ukoko.
  10. K. Kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana.
    Kinyozi hajinyoi na akijinyoa hujikata.
  11. L. Lisemwalo lipo:- Ikiwa halipo, lipo nyuma linakuja.
    Lisilokuwepo moyoni halipo machoni.
  12. M. Mcheka kilema hafi bila kumfika
    Mficha uchi hazai.
  13. N. Nnzi kufa juu ya kidonda si haramu.
    Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kapu ukavune.
  14. P. Penye uermbo ndipo penye urimbo.
    Penye mafundi hapakosi wanafunzi.
  15. R. Radhi ni bora kuliko mali.
  16. S. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utayokytana na mkweo.
    Sumu ya neno ni neno.
  17. T. Tamaa mbele, mauti nyuma.
    Tonga si tuwi.
  18. U. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliyenona.
    Ulipendalo hupati, hupata ujaliwalo.
  19. V. Vikombe vikikaa pamoja havina budi kugongana.
    Vita vya panzi ni furaha ya kunguru.
  20. W. Wema hauozi.
    Werevu mwingi mbele kiza.
  21. Y. Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyomo na yajayo.
    Yote yangáayo usidhani ni adhabu.
  22. Z. Zimwi likujualo, halikuli likakwisha.

8 comments:

  1. zingine zina mantiki lakini zingine ni uzushi kwa kwenda mbele, lol!

    ReplyDelete
  2. Shukrani kwa kunikumbusha Methali na misemo kadhaa!

    ReplyDelete
  3. Ahsante dada Yasinta kutukumbusha. Methali,misemo, nahau na nukuzi ni hazina..uzuri ni kwamba hazichuji na kupoteza maana!

    ReplyDelete
  4. naungana na chacha hakika zingine zina maana ila zingine wizi mtupu.

    ReplyDelete
  5. Haya ngoja na mimi niongeze mojawapo...sikio la kufa...

    ReplyDelete
  6. Asante dada Yasinta kwa hayo. Lakini je, utatuletea lini vitendawili?

    ReplyDelete
  7. kwa majaliwa:
    pampaluma mlango wa chuma ukifunguka hauna huruma .....

    ReplyDelete
  8. Ndugu zangu Haraka haraka haina baraka. Subirini mengi yatakuja. Ntajitahidi sio kubagua ....Ahsanteni.

    ReplyDelete