Friday, October 2, 2009

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MAMA

Mama leo ni siku yako ya kuzaliwa. Twakupenda mama yetu , na twajua kimwili haupo nasi na twaamini kiroho upo nasi. Leo ningekuwa Ruhuwiko ningekuja Mkurumo kushinda nawe. Ama ungekuwa bado u nasi kimwili ningekupigia simu na kukupongeza kwa siku hii ya kuzaliwa na halafu tungecheka kama tulivyokuwa tukicheka. Tunakukumbuka sana na pia tunakutamani sana.

Baada ya kusikiliza mziki huu nikakawa nimeguswa sana. Nikeona si mbaya kama nikiweka hapa kwani najua wote tuna ujumbe mmoja. HONGERA SANA MAMA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA LEO UNATIMIZA MIAKA 57. HONGERA MAMA NAJUA UNANISIKIA.

Ngoja kwa pamoja tusikilize ujumbe huu

9 comments:

  1. Naomba nami niunganishe salamu zangu za heri kwa mama yetu dada yangu Yasinta.

    Ni nani kama mama?
    Hakuna alosimama!
    Hata kama wakisema
    Hawatamfikia mama

    Mama ayajua yote
    Akubali shida zote
    Hata niende popote
    Anitaja kwa wote

    Sasa hayupo mama
    Kaniacha nimeinama
    Wengine wananisema
    Nilimtegemea mama

    Napiga moyo konde
    Napita kwenye mabonde
    Makini nisijiponde
    Nitakuja muona mama!

    ReplyDelete
  2. Naamini huko aliko amekusikia dada....

    ReplyDelete
  3. nami niongeze jambo dada yasinta
    tumboni kwa mama sote tumekaa,
    kifuani kwake tumekula,
    bila yeye tusingejua mapendo,
    hakuna kama mama.
    naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  4. Ni jambo la kusikitisha kwamba tunasherehekea siku ya kuzaliwa mama, wakati mama mwenyewe akiwa hayupo, ametangulia mbele ya haki...Lakini yote yalikuwa ni mapenzi ya mungu hilo litokee ili maisha yaendelee..

    ReplyDelete
  5. Mlongo Mama aliko nauhakika kabisa amekusikia na umefurahi kusikia kuwa unaikumbuka siku hii yake ya kuzaliwa. Ubarikiwe

    ReplyDelete
  6. Na asherehekee akipumzika kwa amani kwani aliowaacha wanaendeleza vema yale aliyowafundisha na ni msaada kwetu sisi (Jamii)
    Pumzika kwa amani zaidi na zaidi Mama

    ReplyDelete
  7. Usilie dada Yasinta, usilie kwani mama yupo nawe na amekuletea watu wengi kwaajili yako. Mbona amekuletea Kamala, Fadhi,Bwaya,harieth, Koero,Mwaipopo,Mwanasosholojia,Kaluse,Ramso,Kissima,Mutibwe, markus,na wengine weeeeengiiiiii sana wapo kwa ajili yako.Mungu yupo nawe na marafiki wameletwa kwako

    ReplyDelete
  8. Napenda kuwashukuru wote kwa kuwa nami katika siku hii maalumu kwa mimi na hasa kwa mama yangu. Ni kama nilivyosema hayupo nasi kimwili lakini naamini kiroho yupo nasi. Sasa ninaamini kweli ninyi sio wanablog wenzangu tu ni ndugu pia na najivunia kwa hili. NAWAPENDENI WOTE.

    ReplyDelete
  9. Jamani, mama, nilikuwa kwenye pilika za maisha, nimekawia nalikini nimefika kukupongeza sina budi HAPPY BIRTHDAY MAMA

    ReplyDelete