Friday, October 2, 2009

HATIMAYE MZEE WA LUNDUNYASA, AANZISHA BLOGU NYINGINE

Mzee wa samaki au mzee wa kuvua samaki hatimaye kaanzisha blog Mpya. Hii ni kwa mujibu wake baada ya tafakuri yamuda mrefu. Karibuni alikuwa kipitia hudma za wordpress lakinihakufanikiwa kuanzisha blog hapo, badala yake ameamua kuendelea kutumia huduma za blogger.

Blog yake hiyo mpya inaitwa http://www.fananinyasa.blogspot.com/. ambayo itakuwa ikizungumzia mambo mbalimbali isipokuwa kuhusu nyasa. Katika blog hiyo kutakuwa na makala zake zinazotoka katika magazeti mbalimbali ya Bongo kama MwanaHalisi, Fahamu, Tazama na KwanzaJamii.

Kwa mujibu wa mzee wa Nyasa ni kwamba ameona ni wakati bora zaidi kufanya hivyo ili kuendeleza kipaji chake cha uandishi wa makala. Hapo ndipo utakapoweza kumfahamu zaidi Markus Honorius badala ya yule Markus Mpangala wa Lundunyasa. Inawezeakana usielewe lakini jina kamili la huyu bwana ni MARKUS DAUDI HONORIUS MPANGALA.

Kwani anaita blogu hiyo FANANINYASA? i FANANI= ni msimuliaji, NYASA= ni kwao mwambao wa ziwa nyasa katika kijiji cha Lundu. kwahiyo ni msimulizi kutoka nyasa. Naamini wanablogu watamwunga mkono, lakini lundunyasa itabaki kama ilivyo ila itazingatia sana mambo ya nyasa na RUVUMAnI hayo tu

Markus Daudi Honorius Mpangala
Maliwa Avenue-Monesteri,
Lundu, Mbinga Magharibi
Ruvuma.

12 comments:

  1. Twaja kwa fanani
    Sasa ile ya Ludunyasa ndio kaitupa ama?
    Kwanza tupe wasifu wake . Hahahahahaaaaaaaaaaa
    Haya sasa, kuzaa si kazi, kazi kulea mwana
    Twakusubiri Markus utuoneshe kilichokusukuma kufungua FANANI NYASA

    ReplyDelete
  2. Kaka siwezi kuitupa lundunyasa nyasa yangu, ila naona kuna baadhi ya mambo nayachanganya na kuiweka blogu hiyo iwe nje ya msingi wa karibuni nyasa. hapa Fanaini anakuja siasa, mapenzi na mambo ambayo naona hayatakiwi kuwepo lundunyasa. kwahiyo kaka Changamoto mzee wa Rasta and Resisatance usijali. Katika fanani utasoma makala zangu kadhaa ninazozitoa katika magazeti mbalimbali na zile ambazo hazitoki magazetini. hapa ni uli ngo wa tabia nyingine ya ya zee la nyeti la nyasa. KARIBUNI mitindo huru

    ReplyDelete
  3. Tumeongeza blog katika familia. Swaaafi

    ReplyDelete
  4. kaka tunaukaribisha ujio wako mpya....

    ReplyDelete
  5. Hongera kuamua kupanua wigo. Karibu sana kaka!

    ReplyDelete
  6. Markus naona umepokelewa na wote na pia naona umeshaanza kazi yako. Mwana wa kunyanja kazanayi kutupela elimu tuvangi.

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  8. waaaaaohhhh markus a.k.a mutu ya nyasa,mutu ya nyumbani hiyo iko juu ile mbaya,mmmmmmh vipi maana toka nikuache kule nyasa upo mdogo sana ulikuwa nanyonya kipindi hicho.nakumbuka ulikuwa unapenda sana uji wa mihogo.mmmm leo nahisi utakuwa mkubwa saaaana.kwa maana karibia unaoa au sio..mmmm mutu ya nyasa uko juuuuuuuuuuuuuuu.kyee kanono pundema pani habi bantu ngababo. mmmh.w r toghether mkuu usijali sikuona blog yako.

    ReplyDelete
  9. eeeee bwana mutu ya nyasa maisha na mafanikio ni mipango na mikakati ya mtu bwana ,usitegemee maisha bora akuletee mtu mwingine ila ni wewe tu jinsi utakavyojipanga ili kupambana na maisha hayo bwana kwani mtegemea cha nduguye hufa masikini.kamua mutu ya nyasa usitumie iriziiiiiiii

    ReplyDelete
  10. we mutu ya nyasa kuna kitu umeniboa mieeee,juzi tui umeenda nyumbani hata dagaa nyasa hujabeba,ila umekuja na vituko kibao,sasa hivo vituko vyako tuvisoma huku midomo yetu ikiwa imekauka?mmmh ila we mtoto mara fanani nyasa,mara nyeti za nyasa toooooba.powaaa bwana karibu sana njombe labda naweza kukufungashia gunia la baridi ili upunguze utundu

    ReplyDelete