Sunday, September 20, 2009

NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA KWA UJUMBE HUU!!!!!

Furaha:- Inakuja wakati kazi zetu na maneno yetu yanapokuwa na faida(fadhila) kwa wewe binafsi na pia kwa wengine.

Amani:- Kuleta amani kwa kila mtu, inabidi kupambana ili kuweka amani yako ya maisha yake pia.

Ushujaa:- Kutokuwepo na woga au kukata tamaa, isipokua ni uwezo wa kushinda.Utulivu:- Ni amani inayokuja wakati nguvu zipo ndani ya upatanifu wa kirafiki upo sawasawa.

Upendo/Mapenzi:- Ni msukumo ambao tumepewa, mapenzi ni pumzi ya maisha juu ya moyo na yanaleta madaha/uzuri ndani ya roho.Bila kusahau ya kwamba upendo una mamlaka , enzi, amri na nguvu hapa duniani.

Busara:- Elimu, kipaji/uwezo wa kuelewa/kuhisi kitu haraka na uzoefu wa mchanganyiko wa kuelekezana na kufikiri jambo/tendo.

2 comments:

  1. Da Yasinta twakushukuru sana kwa ujumbe muruwa wa siku ya Jumapili ya leo. Ujumbe wako umekwenda shule kupita maelezo.
    Nami nakutakia Jumapili njema na Idd Mubaraka.

    ReplyDelete
  2. Ahsante Fadhy mtani! mie jumapili yangu ilikuwa njema kiasi kwani kulikuwa na mvua na kaubaridi hivi. Ila namshukuru Mungu kwa yote

    ReplyDelete