Thursday, September 17, 2009

HATUA SITA ZA KUSAIDIA KUDHIBITI MIMBA SHULENI

MAANDALIZI ya safari yangu kwa ajili ya kumpeleka mtoto wa dada yangu kujiunga na masomo ya sekondari Morogoro yalikwenda vizuri na asubuhi yake nilijona mtu mwenye bahati.

Tulifika mapema kwenye kituo kikuu cha mabasi, Ubungo na tulipokuwa tunaelekea kwenye basi moja ambalo tulitaka kukata tiketi, tuliwaona wasichana kadhaa walioonekana kuwa ni wanafunzi, ni kweli nao walikuwa wanakwenda katika shule hiyo. Alikuwepo mwanamume mmoja aliyevalia vizuri ambaye alijitambulisha kuwa mwalimu wa shule hiyo.
Mwalimu huyo, ambaye alikuwa na vitambulisho vya kazi aliwaambia wazazi waliokuwa wanawasindikiza watoto wao wasisumbuke kwani yeye ametumwa kwa ajili hiyo. Hivyo, wazazi, walezi na sisi wengine tuliotumwa tulimkabidhi mwalimu huyo watoto nasi tukarudi nyumbani.

Kwa haiba aliyokuwa nayo mwalimu yule, kwa umri wake na hata upole alioonyesha, alivyokuwa anazungumza taratibu na alivyotuaminishia usalama, haraka tulinong’onezana kuwa ni mlokole. Niliporudi nyumbani asubuhi ile niliwachekesha wazazi wake kwamba 'nimekbidhi binti yao kwa mwalimu mlokole'.
Hilo lilikuwa kosa kubwa. Utaratibu ule ulikuwa tofauti na fikra zake moyoni, alikuwa mbwa mwitu. Mwalimu huyo ambaye, nahifadhi jina lake, ndiye alikuja kutupa pigo kubwa kwa kumkatisha masomo binti yetu baada ya kumpa ujauzito. Tumefungua kesi kortini.

Pamoja na kuchukua hatua hizo, tumekuwa tukijiuliza nini ki kifanyike ili, siyo tu kwa sisi kupata haki kutokana na binti yetu kupewa ujauzito na mwalimu anayepaswa kuwa mlezi wake, bali pia kuwadhibiti walimu wengine wa kiume wenye tabia ya kuwarubuni wanafunzi wa kike na kuwapa mimba.
Hii ni kwa sababu tuliokumbwa na kero siyo sisi tu bali wazazi wengi, na kumekuwa na malalamiko kila kona unayopita, kuhusu wanafunzi wa kike kukatishwa masomo baada ya kugundulika wamepata ujauzito shuleni.
Japokuwa baadhi ya wasichana hupewa mimba shuleni na wanafunzi wenzao wa kiume, watu wa mitaani pamoja na wafanyakazi, ukweli ni kwamba wengi wao hukatishwa masomo kwa kupewa mimba na walimu wao.
Taarifa mbalimbali na uchunguzi uliofanywa katika maeneo mengi, walimu wanahusika kwa kiasi kikubwa. Walimu hao huwapata wanafunzi kwa urahisi kwa vishawishi kadha wa kadhaa vikiwemo vya kuongezewa alama, kupewa maswali ya ziada (twisheni) na kupangiwa kazi nyepesi.

Kuna ukweli pia kwamba baadhi ya wasichana hupata ujauzito kutokana na kutokuwa na maadili mazuri, papara au ulibukeni wa maisha lakini wengine hulazimika kujenga mahusiano ya kimapenzi na walimu wao kwa kufundishwa masomo ya ziada ili wafaulu mitihani yake.
Kwa mfano, hivi karibuni, tulisikia katika baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa mwalimu mkuu wa shule moja iliyoko Kusini mwa Tanzania amepandishwa kizimbani akikabiliwa na shtaka la kumpa mimba mwanafunzi wake.

Katika tukio kama hili, kwa hali ya kawaida unaweza usiamini wala kupata picha inakuwaje, lakini ndiyo hali halisi ya maisha yalivyo katika ulimwengu wa sasa. Kama mzazi wa kiume anaweza kujenga uhusiano wa kimapenzi na mtoto aliyemzaa sembuse mwalimu?.
Ukichunguza kwa makini utagundua chanzo cha tatizo hili ni tamaa ya walimu na ukiukwaji mkubwa wa kanuni za maadili kazini. Walimu hupaswa kuwa walinzi wa wanafunzi na waongoza maadili kinyume cha hivyo ni utovu wa nidhamu.

Mapendekezo yangu.

Kwanza wazazi wote wenye wanafunzi wa kike wahakikishe wanafungua kesi dhidi ya wahusika ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Endapo binti atadai hajui, kwa lengo la kumficha mhusika, basi binti huyo ashitakiwe binafsi.

Pili, wazazi tusikubali vishawishi vya wavulana au walimu au watu wengine weyote walihusika kwamba wasishtakiwe ila waachiwe wawatunze mabinti na ujauzito walionao. Imebainika hufanya hivyo kwa muda tu, baada ya miezi michache huwapa talaka na huo unakuwa mwisho wao.

Tatu, napendekeza serikali iweke uzito kwa upande wa walimu kwamba watakaobainika kuhusishwa tu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi waachishwe kazi. Nina uhakika hakuna anayependa kuachishwa kazi hivyo wataachana na tamaa yao kwa wanafunzi.
Hatua hizo zinaweza kuchangia kupunguza kuwepo kwa matukio kama haya na walimu watajitahidi kuishi juu ya tuhuma za kimapenzi.

Nne, uwepo utaratibu wa kuwapima wanafunzi wa kike kila mara na kuwapa ushauri nasaha kwamba wajifunze na wazoee kusema "hapana" wanapofuatwa na walimu wao kimapenzi.

Tano, iko haja ya kuweka sheria kuzuia wanafunzi kufika kwa walimu kama hawana uhusiano wa kidugu. Shule za seminari na zinazoendeshwa na masista zimeweza, kwa nini ishindikane katika shule za serikali?

Sita ni kwamba chanzo kingine cha matukio ya mamba ni kushiriki starehe. Wazazi wawazuie watoto wao; wavulana kwa wasichana kujiingiza kupita kiasi kwenye burudani kwani ni nchimbuko kubwa la maasi ya maadili na mwishowe kupeana mimba.

Hii ilitoka mwananchi la tarehe 23/6/2009 na mwandishi Elizabeth Suleyman.

11 comments:

  1. Kusema kweli swaa la mimba mashueni lina pande mbili, ingawa watu hawataki kukubali, kwanza wanaume wanaowahadaa vibinti vya shule au wanafunzi wa kiume wanowahada wanfunzi wenzao wa kike na pili mabinti wenyewe.
    Ingawa kuna kelele nyingi san zinazopigwa dhidi ya wanaume, lakini naomba tukubaliane kuwa vibinti navyo viahusika katiak jambo hilo kwa njia moja ama nyingine. kwanza mavazi yao wanayovaa sio ya kijisitiri na pia kutumia muda wa usiku kutembelea katika kumbi za staehe pamoja na kutaka maisha ya hali ya juu yasiyolingana na vipato vya wazazi wao au walezi wao....wao ndio wanaokuwa wawindaji wazuri wa wanaume ili kujipatia kipato cha ziada.
    Sikatai kuwa wapo wanaume ambao kwa makusudi huwahadaa mabinti wa shule na kuwajaza mimba na kisha kuwakimbia, lakini ni vyema jambo hili likatazamwa kwa mkabala tofauti.

    ReplyDelete
  2. sioni tatizo la mimba kwani bila mimba mimi nisingekuwepo bila kujali kama mama alidanganywa, alibakwa au alilazimishwa. mimi nafurahia kitendo hicho kilichomsababisha mama kupata mimba vinginevyo tusingefahamiana.

    ReplyDelete
  3. kamala unachanganya mada, hapa dada yasinta hakuzungumzia kuwa mimba ni mbaya au nzuri, mjadala hapa ni kuhusu athari zinazotokana na wanafunzi kubebeshwa mimba wakingali wanasoma. kama tutasema mimba ni nzuri ina maan ni kuwakwamisha watoto wa kike kujipatia elimu, kwani wakati watoto wa kiume wakiendelea na masomo wale wakike wanlazimika kusimama kwa sababu ya kupata mimba..hata kama wameruhusiwa kuendelea na masomo, uwezekano wa kusoma kama wanfunzi wengine utakuwa ni mgumu na huenda hata wakafeli kutokana na matatizo ya ujauzito.
    Kwa hiyo kamala Mimba sawa lakini zisubiri basi tumalize masomo.....

    ReplyDelete
  4. wewe koero, kipi kizuri kati ya kuzaa na kusoma? mtoto ni mtoto bwana. bora kuzaa kuliko shule. mwanamke aliyezaa ni mtu wa nguvu duniani. kakamilisha uumbaji wa Mungu. unamaanisha wasiosoma hawazai? basi tutafute jinsi ya kuwaondolea muwasho wakiwa shule.

    kimaumbile ni bora kuzaa kuliko kusoma na akizaa anajifunza mengi kuliko vitabu vya darasani. sioni tatizo

    ReplyDelete
  5. Kamala ngoja nikunukuu:

    'kimaumbile ni bora kuzaa kuliko kusoma na akizaa anajifunza mengi kuliko vitabu vya darasani. sioni tatizo'
    Mwisho wa kunukuu...

    kaka yangu kamala naona wewe unataka kupotosha watu hapa....wakati wenzako tunatumia ubongo kufikiri...sijui wewe unatumia kitu gani...LOL

    Hivi kuzaa ni kujifunza kitu gani, mbona hata wanyama wanazaa, je ni kitu gani wanajifunza wale?
    Niliwahi kuona makala moja pale kibarazani kwako tena uliambatanisha na picha ukifundisha, Je hiyo ndiyo elimu uliyokuwa ukiwafundisha wanafunzi wako......Loooooh! nawasikitikia...
    Let us be serious, tuizungumzie mada hii kwa kujenga na sio kwa kukejeli,,,kumbuka kuwa nawewe una mwenzi wako na utakuja kuwa na watoto, natamani uzae watoto wa kike halafu kauli yako hiyo ikurudie....naamini utakuwa na utitiri wa wajukuuu usiojua baba zao......eti kuzaa ni kujifunza mambo mengi.....LOL shame on you......

    ReplyDelete
  6. Mimi huwa napinga sana suluhisho lolote linalohusisha jela, sijui adhabu kali, sijui hatua kali za kisheria na kadhalika. kama sheria zipo jamani, nakumbuka miaka ile tunasoma elimu ya huko ambako kupata mimba ni kosa kulikuwa na sheria kwamba anayemmimbisha mwenzake basi adhabu yake ni jela miaka saba, lakini je watu waliacha kufanya hivyo? bado tu, tutafute mbinu zingine za kulishughulikia hili badala ya kukimbilia hatua kali za kisheria, hizo zipo kila siku na siku hizi ndio hazitishi kabisa!!
    Jambo lingine ni kuangalia pia upande wa pili, hawa wanaopinga wajiulize wao walianza lini hii michezo, na kama walichelewa kuanza walijitunza vipi, nadhani hizo elimu ni muhimu zaidi kuliko kujazana ujinga wa "hatua kali za kisheria". Sheria zipo na watu tunazijua. Elimu ya maumbile iongezwe!!!

    ReplyDelete
  7. Mimi nadhani nguvu kubwa ielekezwe kwa watoto hawa wa kike.Katika hatua za wanaume wakware kuwa karibu na wanafunzi hawa wa kike naamini wanafunzi hawa huwa wanakutana na usumbufu mkubwa sana,ambapo wakati huu ndio muafaka kabisa wa kuripoti juu ya usumbufu wa mwalimu na wanaume wengine wakware.Najiuliza,kama mtoto huyu wa kike hafagilii then kwa nini akae kimya?Ni kweli kwa kila aina ya udanganyifu hajui mwisho wake nini? Kama ndivyo, lawama kwa wazazi/walezi lazima ziwaangukie.Kama wazazi/walezi hawatawafundisha watoto wao kuhusu mambo haya basi watoa wasaa kwa vijana hawa kufundishwa na ulimwengu na ndio maana wengi huwa wanajifunza baada ya kuathirika.

    Dada Yasinta, ningependa kama ungemuuliza(pengine mlimuuliza) huyu mwanafunzi kwamba baada ya kuona mwalimu huyu anamfuata fuata na kuonyesha kila dalili za kumtaka kimapenzi yeye alichukua hatua gani, ni mambo gani yaliyomridhisha mpaka akaridhia kuwa na uhusiano wa kimapenzi na huyu mwalimu.
    Kama alibakwa tujue, na kesi isiwe tu ya mwalimu kumjaza mimba mwanafunzi bali pia atuhumiwe kwa kosa la kubaka.

    ReplyDelete
  8. Asanteni wote nami ngoja niseme machache. Mnajua huwa nakasirika na naumia sana kuona hili jambo haliishi yaani tangu nimepata akili nasikia tu wanafunzi wanafukuzwa shule bla bla bla. Baba mzima ana mke na watoto nyumbani lakini anadiriki kumpa mtoto wa mwenzake mimba na kuyafanya maisha yake yaishia hapo.

    Kwa nini wanaume hawawezi kujizuia kwa nini kuchagua watoto wa shule na sio kutafuta wanawake wazima wenye kujua mimba ni nini? maana pale yule mtoto anapata mimba na akizaa hajui hata kumtunza mtoto wake ambaye ni mtoto mwenzake hata kumwogesha hawezi.

    Kama mmoja alivyosema inatakiwa haraka sana watoto wapata soma la elimu ya Uzazi pia viungo vya miili yao kwani sasa hali inazidi kuwa mbaya mno. Na serikali ndiyo ya kulaumiwa kwani hao walimu inabidi afukuzwe kazi kabisa. Wafanyacho ni kuwahonga wanafunzi usipolala nami utapata max ndogo au utafeli mtihani na mwanafunzi kwa kuogopa anakubali. Kweli huu ni uungwana? .....

    ReplyDelete
  9. Da Yasinta, ni kwa nini na hao mabinti wanajirahisisha pia? Wakiombwa kumegwa wanapagawa ka nini sijui...lol!

    Da Koero, kwamba KL atakuwa na wajukuu wasojua baba zao sidhani kama ni kweli kwani ajuaye baba wa mtoto ni nani mama...lol

    yawezekana na mimi huyu nnayemuita baba siye...lol

    ReplyDelete
  10. Chaha Wambura!! Inawezekana kutokana na udhaifu wetu au mazingira waliyolelewa. Na kwa nini wanaume wanataka mabinti wadogo? Ni kweli inawezekana siye babako...LOL

    ReplyDelete

  11. Kutana na mtaalamu WA mitishamba dr toka tanga anazo dawa za uzazi ..ugumba...kukuza hips shape na makalio..kukuza uume na kunenepesha.kupata watoto pacha ...anatibu bawasiri . UTI sugu...mpigie kupitia 0744903557 dawa zake ni mitishamba na anasafirisha popote ulipo Kwa anayehitaj

    ReplyDelete