Thursday, September 24, 2009
DIWANI AFUMANIWA NA MKE WA SHEIKH USIKU WA MANANE
DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tunduru amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mmoja wa masheikh mkoani hapa. Katika fumanizi hilo la aina yake, sheikh huyo alipigwa na butwaa baada ya kumshuhudia diwani huyo akiwa amejifunga kiunoni kitenge ambacho alimnunulia mkewe mara baada ya kubisha hodi.
Tukio hilo limetokea juzi saa nane usiku baada ya mume wa mke huyo kupata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mkewe ameonekana katika nyumba ya diwani huyo (jina tunalo).
Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, diwani huyo alikiri kutokea kwa fumanizi hilo lakini akadai kuwa ni njama zilizopangwa na washindani wake wa kisiasa ili kumchafua.
Baadhi ya watu waliodai kushuhudia tukio hilo walisema kwamba mikakati ya kumfumania ilipangwa na majirani baada ya kuona mke huyo wa sheikh ameingia ndani kwa diwani huyo.
Walidai diwani huyo ana tabia ya kula na wake za watu na hiyo imemjengea uhasama kwa watu wengi kiasi kwamba ilibidi watoe taarifa kwa sheikh huyo ili kumkomoa.
Mara baada ya shehe kupata taarifa hizo aliongozana na mwenyekiti wa kitongoji cha Raha leo, Mkwanda Mussa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Kitani, Nyenje Madefu hadi nyumbani.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, jopo hilo lilipofika kwenye nyumba walimokuwemo ndani na kubisha hodi, diwani huyo alifungua mlango akiwa amejifunga kitenge cha mke wa shehe huyo kiunoni na kuwataka waeleze shida waliyoijia.
Walisema diwani huyo alipigwa na butwa na kuonekana kuwa na kigugumizi baada ya jopo hilo kumueleza kuwa limefika kumtafuta mke wa shehe waliyehisi kuwa yumo ndani.
Kabla hajajibu lolote waliingia ndani na kumkuta mke wa sheikh akiwa amelala kitandani na ikawa ni ushahidi wa kumkamata diwani huyo hadi ofisi za kata ili kumhoji.
Baada ya mahojiano ya muda mrefu, inadaiwa kuwa diwani huyo alikiri kosa la kulala na mwanamke huyo na ikaamuliwa alipe Sh300,000 kama faini kwa sheikh.
Alifanikiwa kupata Sh150,000 na kuahidi kiwango kilichobaki atakilipa hara iwezekanavyo.
Baadhi ya wakazi wa kata anayoongoza diwani huyo, walidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa alio nao kwa ajili ya kula na wake za watu.
Habari hii inatoka Jamii Forum imeandikwa na Joyce Joliga, Songea
Hatari kubwa diwani mzima anafanya vitendo hivyo haya yetu macho na masikio.
ReplyDeleteJamani jamani. Mbona tunafananisha KIFO NA USINGIZI???
ReplyDeleteYaani mtu aliyezini anatoza faini ya pesa? Ili akaendeleze uzinifu?
Mie sijui NJAA itatufikisha wapi. Amegharamia vipimo vya magonjwa ya zinaa na UKIMWI? Ama mume anaenda kununua shuka jipya kwa hizo laki tatu na kisha "kubanjukia" na mzinifu wake?
Mie naacha
DUH!
ReplyDeleteKwa hiyo Mke wa shekhe ni shilingi laki tatu kufumaniwa mara moja hata kama nyama ya bata ililiwa angalau kwa miaka mitatu mara mbili kwa wiki?
Mmmmh!:-(
Mengine Mzee wa Taratibu na Mzee wa Changamoto Mshayasema!
Hii haijatulia kabisa,labda niulize swali,huyo shekhe ana wake wangapi? na huyo mke aliyefumaniwa ni wangapi?hapo kweli ukimwi utakwisha? hao hao madiwani ndio wanajidai kuhamasisha watu wajiepushe na ukahaba,sasa hapo anatoa mfano gani?
ReplyDeleteNdipo hapoutagundua watu na masuala ya uaminifu katika ndoa hakuna, Sheikh wa watu kakimbilia faini. Na bado lazima amkatie mjumbe pesa ya usuluhishi. Wakuu hapo juu wamenena kiasi cha kutosha. Thup, nimetema mate kwa uozo huo.
ReplyDeleteNdipo hapoutagundua watu na masuala ya uaminifu katika ndoa hakuna, Sheikh wa watu kakimbilia faini. Na bado lazima amkatie mjumbe pesa ya usuluhishi. Wakuu hapo juu wamenena kiasi cha kutosha. Thup, nimetema mate kwa uozo huo.
ReplyDeleteNikweli hapo inaonekana pesa ni mali zaidi kuliko mke. Wanaume hawana maana kabisa. Samahani kama hii sentensi itawakwanza wengi.
ReplyDeleteAsanteni kwa kutochoka kutembela maisha .
Mh!
ReplyDelete