Monday, August 3, 2009

WATOTO NA TATIZO LA KUSHINDWA KUSOMA

Wapo baadhi ya watoto ambao hutokea kutokuwa na uwezo wa kusoma kabisa. Hali hii inaweza kutafsiriwa kama kitendo cha mtoto kutokuwa na uwezo wa kiakili, wa kuweka kumbu kumbu na kuta taarifa katika maandishi, kwa maan ya kutokuwa na uwezo wa kusoma na kuandika, na hivyo kuwaweka wazazi katika wakati mgumu wa kutojua mustakabali wa maisha ya mtoto wao.

Inasemekana kuwa watoto wa aina hii huwa wanakuwa na kuiwango cha kawaida, cha chini na hata cha juu cha akili. Tatizo hili kwa kiwango kikubwa huwa linawatokea zaidi watoto wa kiume, ukilinganisha na watoto wa kike, na kitaalamu hujulikana kama Dyslexia.

Watoto wenye tatizo hili hupata ugumu katika kutumia lugha fasaha kwa maana ya kutoweza kusoma neno kama lilivyoandikwa. Kwa mfano anaweza kusoma neno mutaskabali akiwa na maana ya mustakabali au kuandika namba 548 badala ya 584,au wakati mwingine kuandika L akiwa na maana ya namba 7.

Je wazazi watawatambuaje watoto wao wenye tatizo hili?Mara nyingi watoto wenye tatizo hili huwa wanapuuzwa, hivyo kuwa vigumu kuwatambua kwamba wan tatizo hili. Na huw ahawpewi msaada maalum kwa kuonekana kwamba tatizo walilonalo ni la kawaida tu, baadae watajua kusoma na kuandika.

Watoto wenye tatizo hili huwa wanajitanabaisha kwa dalili zifuatazo:

1. Huwa ni vigumu sana kwao kujua kusoma, 2. Wanaposoma wanasoma ovyo ovyo. 3. Wengine hawakumbuki wamesoma nini kwa vile akili yao yote inakuwa maneno sio herufi. 4. Wanakuwa na matatizo ya kuandika/kupanga herufi sawa sawa.

Zipo njia mbalimbali za kuwasaidia watoto wenye tatizo hili. Ni muhimu kwa jamii kutowachukulia kama hawana akili kabisa, kwani kitaalamu watoto wa aina hii wanakuwa na kiwango cha kawaida au kuzidi kawaida. Hivyo kinachotakiwa kwa wazazi na waalimu ni kuwapa msaada wa ziada ukilinganisha na watoto wengine wasiokuwa na tatizo la aina hiyo.

Kwa mfano wazaziwanaweza kutafuta mwalimu ambaye atakuwa anakuja nyumbani kumfundisha mtoto mwenye tatizo hilibaada ya saa za kawaida za masomo. Na mara nyingi zoezi hili linapofanyika linatakiwa lisimjengee mtoto hisia kwamba yuko tofauti na watoto wengine, kwani kwa kufanya hivyo kutamjengea mtoto huyo kutokujiamini na mwishowe kushindwa kabisa kumudu kusoma

8 comments:

  1. Ahsante da Yasinta kwa elimu nzuri. Kumbe watoto hupuuziwa wakati ni jambo la kupewa umuhimu.
    Ni darasa zuri sana.

    ReplyDelete
  2. Elimu nzuri hii.
    Ni vizuri kabla hujamuita mtoto kuwa ni zezeta na hafundishiki kwa kuchunguza kama ana matatizo ya kiafya ambayo anaweza kusaidiwa kwa wataalamu husika.
    Kumfurumua tu ni kumuongezea matatizo ya kisaikolojia juu ya tatizo ambalo tayari analo.

    ReplyDelete
  3. Unafaa kuwa mwalimu kwani elimu ambayo umeitoa hapa ni zaidi ya mwalimu

    Hakina hongera kipaji unacho na Wangoni Songea wanajivunia siku walimu wakigoma bila shaka darasani utaingia kuziba pengo

    ReplyDelete
  4. Unafaa kuwa mwalimu kwani elimu ambayo umeitoa hapa ni zaidi ya mwalimu

    Hakina hongera kipaji unacho na Wangoni Songea wanajivunia siku walimu wakigoma bila shaka darasani utaingia kuziba pengo

    ReplyDelete
  5. Dada umetoa darasa zuri sana, hata mie nilikuwa na upeo mdogo katika jambo hili.Asante kwa maelezo mazuri.Hivi wewe ni mwalimu nini? maana mambo yako makubwa!

    ReplyDelete
  6. Ni darasa zuri dada,
    hata mimi nimejifunza kitu hapo...

    ReplyDelete
  7. Ni kweli ni elimu nzuri asanteni wote kwa kuwa nami na kuto choka kunitembela na kunipa moyo.

    Kuna jambo nimekumbuka sasa hivi tu ni kwamba hapa watu/watoto waiojua kusoma husaidiwa yaani wanakuwa na mwal.maalumu kwa ajili yao. Halafu jingine ni kwamba hata mfalme wa hapa Sweden ana shida hiyo. Ni hayo tu na tupo pamoja

    ReplyDelete
  8. Kuna wakati nafikiri wanaoshindwa kuelewa kuwa watoto hawa hawana matatizo ndio wenye matatizo. Nadhani hapa linalowakwaza ni mwendokasi wa ubongo kupokea lakini si ulemavu.
    Ni sawa na mtu kuvua nguo ukiwa umefumba macho ukiamini kuwa kwa kuwa huwaoni, basi hawakuoni.
    Yawezekana ni mfumo tuu wa kutumia UKUBWA kuwaona wao wana makosa, ilhali mkubwa ndiye asiyeona tatizo.
    Labda tuwakumbushe kuwa NAMNA UONAVYO TATIZO NDIO TATIZO

    ReplyDelete