Hapa vipi?
Sijui kama wenzangu mmewahi kujisikia hivi, mwenzenu leo nimeamuaka na kujiona ya kwamba:- Ninaringa kwa kuwa mtanzania nchi yangu yenye sifa zote za ustaarabu.Ninaringia rangi yangu nyeusi, macho meupe, ngozi yangu nyororo, ninapendeza na nywele zangu nyeusi na kiswahili ni lugha yangu.
Ninajivunia nchi yangu ya Tanzania yenye miji ya kuvutia iliyojengeka. Angalia Dar es salaam, Mwanza nayo Dodoma bila kusahau kwenye marashi mji wetu Zanzibar. Halafu ukienda Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Songea.
Mnajua kuna vivutio vingi ndani ya Tanzania vinavyotufanya sote tujivunie kwa mfano kuna bahari fahari ya Taifa, Ziwa nyasa, viktoria, Tanganyika pia mlima mkubwa barani afrika Kilimanjaro. Bila kusahau mbuga za wanyama Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Mikumi n.k
Hongera sana kwa kuwa Mtanzania halisi.
ReplyDeleteNakuunga mkono...najivunia pia
ReplyDeleteNi kweli kabisa...Tanzania,pamoja na umasikini na karaha mbalimbali wanazokabiliana nazo wananchi wa kawaida,ni nchi ambayo imesheheni mengi ya kujivunia.Naungana nawe.
ReplyDeleteI think you have "home sick" mdada inabidi uende kunyumba ukawasalimie.
ReplyDeleteWell sikujua kuwa wewe ni mtu kutoka RUVUMA mie pia ingawa ninatoka Tunduru.
Ndugu au sio.
Binti z
WHO WAS THE LUCKY ONE WHO CAUGHT YOU COMING OUT OF THE SHOWER
ReplyDeleteYasinta kweli umekumbuka nyumbani wewe,kama mdau hapo juu alivyosema ni kweli una "home sick",yote na yote Tanzani ni nchi yakujivunia tunakila sababu ya kujivunia,wengi wanaitamani sana Tanzania yetu.
ReplyDeleteNajivunia Utanzania ila kuna wakati vitu kama mauaji ya Maalbino huwa jasho linanitoka katika hali ya kujaribu kuelewa visivyoeleweka.
ReplyDeleteSwali:
Hivi kwanini Tanzania inasifiwa kwa kila kitu hasa amani mpaka mali asili bila kusahau watu bomba halafu eti bado kiuchumi hata kimichezo bado tunashindana au kushindwa na nchi zilizo vitani?
Kaka Mkodo. Hakuna shilingi yenye upande mmoja. Amani ndio iwafanyao mafisadi "watanue". Upendo (ama niseme unafiki) ndio unaotufanya tutajane tunapokula pesa za vyama vya michezo. Mshikamano ndio unaotufanya tusiseme anayeruhusu kupima viwanja na kujenga Jangwa na kisha kupeleka umeme wakati hakuruhusiwi kuishi watu. Miaka ikishapita mnaambiwa NI HARAMU KUIHSI HUKU.
ReplyDeleteNaipenda Tanzania, Nampenda Yasinta pia. Labda kwa kuwa anaipenda Tanzania na anajivunia visivyovuniwa.
Hivi naeleweka? Naacha
Kuhusu kuipenda Tanzania, labda jina lake tu.
ReplyDeleteHakika dada Yasinta umependeza na unavutia, kweli Tanzania imejaaliwa kuwa na warembo kama dada yangu Yasinta.......
mimi huwa najiuliza tanzania nini na mtanzania ni nani. nilipokuwa mkristo tulimshukuru saaaana Mungu kwa kutupatia tanzania yenye amani na sasa tunamshukuru baba wa taifa, nyerere!
ReplyDeleteswali;
eti tanzania iliumbwa na Mungu? kwa nini tusimshukuru bismark na karl peters waligombana nakuanzisha tanzania tukawaita mababa wa taifa badala ya nyerere aliyekuta mipaka yoote imewekwa kwa ajili yake?
najiuliza tu wakuu