Wednesday, July 29, 2009
BABA NA MAMA, NI NANI AMBAYE HAKUCHEZA MCHEZO HUU?
Katika ukuaji wetu, naamini wengi wetu tumeshiriki michezo mingi ya utotoni.
Mingi ya michezo tulioshiriki ni huu wa baba na mama ambao kule kwetu Songea tumezoea kuuita Madangi.
Mchezo huu wa baba na mama huchezwa na watoto kwa kuwaiga wazazi wafanyavyo kwa kuigiza mambo ya mapishi na mambo ya mapenzi ya kitoto.
Mchezo wa Mapenzi ya kitoto ndio ambao ningependa kuuzungumzia leo. Naamini karibu wote sisi, hakuna ambaye hajapitia mchezo huu. Inasemekana watu saba kati ya kumi miongoni mwetu, hakuna asiyefahamu mchezo huo.
Hata hivyo takwimu zisizo rasmi zinaonyesha kwamba watoto wa kiume ndio wanaoshiriki zaidi mchezo huu wa mapenzi ya utotoni kwa asilimia 85, ukilinganisha na watoto wa kike ambao wao hushiriki kwa kiwango cha asilimia 75.
Mchezo huu kiukweli hauna madhara yoyote kwa kuwa washiriki wote ni watoto, isipokuwa, adhabu na kauli zinazotolewa na wazazi hugeuka sumu.
Hebu fikiria watoto wanafumaniwa na mzazi wakicheza mchezo huu wa mapenzi ya kitoto, mzazi huyo anatoa adhabu ya viboko kwa watoto hao kisha kuwaita watoto hao kuwa ni wajinga na shetani wakubwa kwa kufanya jambo hilo ambalo wakati huo litabatizwa jina la mchezo mchafu na usiofaa kabisa, na mara nyingi kauli hizi kuelekezwa kwa mtoto wa kike, lakini mtoto wa kiume huachwa tu kwani kwa wazazi wengine huonekana ni shujaa.
Mara nyingi kile tulichoambiwa utotoni ndivyo tunavyokichukulia hata ukubwani, kwa hiyo zile adhabu za kuchapwa bakora na kuambiwa kuwa huo ni mchezo mchafu na wa kishetani, hubaki akilini mwetu hata leo na ndio maana tendo la ndoa miongoni mwetu hasa wanawake linabeba taswira ya kitu cha aibu na kisichofaa. Hii inatokana na zile kauli tulizoambiwa utotoni kuwa mchezo huo ni mbaya na wa kishetani.
Wanawake ndio wahanga wa kauli hizi na ndio maana hata wale walioko kwenye ndoa wanakosa uhuru wa kujieleza kwa wenzi wao kutoridhishwa na tendo la ndoa inakuwa ni vigumu. Atawezaje kujieleza wakati alimbiwa kuwa huo ni mchezo mchafu na wa kishetani usiofaa hata chembe kufanywa na mwanaadamu?
Unaweza kukuta mwanamke ameolewa lakini hawezi kuwa huru kumueleza mwenzi wake hisia zake za kimapenzi kwa sababu ya kauli hizi kukaa kichwani na kuhisi aibu.
Kwa hiyo kwa kutumia sauti za wazazi wetu au walezi wetu na sauti ya jamii tunalitazama tendo la ndoa kama uchafu ili hali tunalihitaji na ni muhimu ili tuendelee kuwepo.
Hivi hakuna dalili kuna wazazi hustukia wameshawahi kuchunguliwa ndio siri ya kupaniki kwa kustukia watoto kuna kitu cha fargha wanajua ambacho ni cha zaidi ya kujipikilisha?
ReplyDeleteNgoja ninukuu:
ReplyDelete"Mchezo huu kiukweli hauna madhara yoyote kwa kuwa washiriki wote ni watoto, isipokuwa, adhabu na kauli zinazotolewa na wazazi hugeuka sumu.
Hebu fikiria watoto wanafumaniwa na mzazi wakicheza mchezo huu wa mapenzi ya kitoto, mzazi huyo anatoa adhabu ya viboko kwa watoto hao kisha kuwaita watoto hao kuwa ni wajinga na shetani wakubwa kwa kufanya jambo hilo ambalo wakati huo litabatizwa jina la mchezo mchafu na usiofaa kabisa, na mara nyingi kauli hizi kuelekezwa kwa mtoto wa kike, lakini mtoto wa kiume huachwa tu kwani kwa wazazi wengine huonekana ni shujaa"
Mwisho wa kunukuu,
Hapo dada umenena, kuna siku nilishuhudia watoto wa jirani walikamatwa wakicheza huo mchezo wa kikubwa , lakini walioadhibiwa ni watoto wa kike wale wa kiume waliachwa bila kuguswa....
Huu ni uonevu na ndio maana wanawake huliona tendo hilo kama nuksi na lenye kufedhehesha, aina ya malezi yetu humkandamiza sana mwanamke.
Kama watoto hasa wa kike wakikamatwa wakifanya tendo hilo huitwa shetani, unategemea akifikia umri wa kujamiiana atalifurahia tendo hilo? na ndio maana sishangai kusikia kuwa wanawake ndio pekee huchelewa kufika kileleni, hiyo ni kutokana na zile hisia za kuitwa shetani kumrejea........
Jamani tunaonewa kwa mengi.....
Mmh!
ReplyDeleteAhaaaaaaaaaaaa!!! Sikujua. Ya leo kali wapendwa. Nasubiri maoni nijifunze
ReplyDeleteNdio maana watu wanasema "Children do what you do, not what you say".
ReplyDeleteUmenikumbusha mbali duh!
ReplyDeleteKusema kwel mchezo huo hauna madhara
Ayeee!!!!
ReplyDeleteLakini wazazi ukali wa nini wakati usiku wanalala na watoto chumba kimoja, wanafikiri watoto wajinga!!
Hakika dada Yasinta umenikumbusha mbali maana mie nilikuwa nikiona kinadada wanacheza na mie nangang'ania nicheze, "Aibu".
ReplyDelete