Sunday, July 26, 2009

MAJIBU KWA KAKA BWAYA KUHUSU MIMI "YASINTA"

Hapa ni maombi maalau kutoka kwa kaka Bwaya. Anasema:-Dada Yasinta, mie nina maombi maalumu yafuatayo:

1. Tutajie mambo kumi tusiyoyajua kuhusu wewe. Uamuzi wa yapi unaweza kutuambia, unabaki kuwa wako.

2. Ni watu gani watano huwezi kuwasahau katika maisha yako?

3. Mambo yepi mawili yanatumia muda wako mwingi katika masaa ishirini na mane ya siku?

Nami nimejitahidi kujibu kama ifuatavyo:-

1. Tutajie mambo kumi tusiyoyajua kuhusu wewe. Uamuzi wa yapi unaweza kutuambia, unabaki kuwa wako.

=Mpole kiasi
=Mcheshi
=Mwenye upendo kwa watu wote bila kujali rangi, dini, kabila na itikadi
=Anayejali familia
=Anayependa kujitolea kuisaidia jamii, kwa njia mbali mbali
=Asiyependa majungu
=Mdadisi na anayependa kujifunza mamabo mapya
=Anayependa kuwafundisha wengine yale anayoyafahamu
=Anayependa kusikiliza muziki wa aina mbali mbali
=asiyependa kuona jinsia ya kike ikidhalilishwa kwa sababu ya mfumo dume



2. Ni watu gani watano huwezi kuwasahau katika maisha yako?
=mama yangu na baba yangu
=Mzee aliyenilea nilipokuwa masomoni chuo cha kupiga chapa
=Rafiki yangu aliyenipeleka hospitali nilipokuwa naumwa na mguu baada ya kuchomwa na mwiba wa samaki
=Mume wangu
=watoto wangu

3. Mambo yepi mawili yanatumia muda wako mwingi katika masaa ishirini na mane ya siku?


=Familia na kublog
=Kazi

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!

11 comments:

  1. Duh!! Kama ni kampeni binafsi basi ungeshinda maana umejipigia upatu mkubwa saaana. Sema kwenye swali la pili, mtu wa nne na watano ndio wanaweza kuweka kauzibe kwa wakware (Lol)
    Bwaya ana maswali magumu jamani. Nadhani ningepata wakati mgumu kuyajibu haya. Lakini nafurahi umeweza na nashukuru kuwa nimejifunza kitu.,
    Amani kwako, kwa Bwaya na kwa FAMILIA YAKO PENDWA.
    Bless

    ReplyDelete
  2. Duh kaka Bwaya mgomvi. Lakini kaka yangu Mubelwa hicho cha tano, watoto siyo tatizo, tatizo ni hiyo namba nne.

    Halafu mbona da Yasinta amejieleza sana? Ama ndo mazoezi ya twenty ten?

    Ila kujieleza unajua.

    ReplyDelete
  3. Hapo wala sibishi chochote because you seem like a very nice person

    ReplyDelete
  4. Ewaaaa! Sasa nimemfahamu dada Yasinta kwa uzuri zaidi. Dada Yasinta umesema wewe ni mpole kiasi, ina maana ni mkali wastani au?(hahahaaaaaaa!)

    ReplyDelete
  5. 100% zamani tukiwa UPE ulikuwa unaanikiwa mia ya mia, halau wanazungushia duara na nje ya duara mwl anaandika Vizuri sana.Ndicho ulichopata Yasinta.You are Brilliant!

    ReplyDelete
  6. Atakuwa ni malaika tu! Maana duh!

    ReplyDelete
  7. Du Pole sana kwa huo Mwiba wa SAMAKI!Miiba mingi ya samaki ina maumivu sana,Bahati ulikochoma mguuni,Ingekuwa kooni ungeumia sana Yasinta!.Pole

    ReplyDelete
  8. Asanteni sana.Maoni mazuri WOTE MNAPENDWA.

    ReplyDelete
  9. bora ukawaulize woote wakuchukiao na kuwauliza sababu za chuki na uziandike kuwa ndio wewe!!!!! nnnnooooot

    ReplyDelete