Monday, June 8, 2009

MWANZO WA BINADAMU, MASWALI NI MENGI KULIKO MAJIBU. JE UKWELI NI UPI?

Nimelala leo na kufikiri kwa nini watu tupo tofauti. Lilikuwa swali la kwanza kumuuliza mume wangu leo badala ya kusema umeamkaje? Na baadaye nikakumbuka hii mada ya kaka Shabani Kaluse nikaona ni vema niiweka hapa ili nipate jibu. Kwani hili jambo linanipa utata sana kwa nini kuna waafrika, wazungu, wahindi, waarabu, nk. Kama kweli ni kweli mwanzo wote tulikuwa waafrika bado sijaelewa. Labda sasa nitapata jibu Asante kaka Kaluse kwa mada hii.


Kama nilivyosema wakati nafungua huu mjadala kuwa nadharia ya uwepo wa binadamu imejaa utata mtupu.
Katika dini tulifundishwa kwamba binadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa Adam na Eva, na nilipokuwa shule, napo nilifundishwa kuwa chanzo cha binadamu ni nyani, halafu akawa anabadilika hadi kufikia kuwa binadamu.

Lakini bado kuna Maswali najiuliza, hivi ni kwa nini, nyani wengine wamegoma kubadilika hadi leo? Yaani wamebaki kuwa nyani badala ya binadamu.
Je na sisi kwa nini tumesita kuendelea kubadilika?

Kama tulikuwa kama nyani, halafu tukabadilika na kuwa binadamu, inakuwaje tusiendelee kubadilika zaidi na zaidi? Au kulikuwa na mipaka ya kwamba tukifikia mabadiliko kama haya tuliyonayo iwe ndio basi?

Kama ingekuwa binadamu aliumbwa kama nyani na kubadilika kufuatana na mazingira labda na mambo mengine, mbona basi leo hii uhusiano wa kinasaba kati ya binadamu na nyani sio mkubwa kama ule uliopo kati ya binadamu na panya weupe?
Yaani wale panya niliowaeleza awali katika makala iliyopita kuwa ndio wanotumika kufanyia utafiti masuala mengi yenye kumgusa binadamu, kwani kinasaba panya hawa wanakaribiana na binadamu.

Basi kuna haja ya kuamini kwamba binadamu wa kwanza alikuwa ni panya kisha akabadilika na kuwa kama alivyo leo.
Lakini bado najiuliza kwa nini huyu panya asiendelee kubadilika, amefungwa na kitu gani?


Hivi karibuni wakati naperuzi peruzi katika mtandao nimekutana na mijadala mikali kuhusu asili ya viumbe hai.
Kwa mfano nchini Marekani mjadala huu umeingia mashuleni ukiwa na nguvu mpya, kutokana na vijana wengi nchini humo kupambazukiwa na kukataa kukaririshwa elimu za wanasayansi wa kale zisizo na mashiko.

Vitabu vingi vya Baiolojia vilikuwa vikisema kwamba asili ya viumbe hai ni mwendelezo wa mabadiliko (Evolution)
Walimu wengi wa nchini Marekani na Ulaya ambako jambo hili limeshika nguvu wanapinga nadharia hii ya mabadiliko na wanaamini kwamba viumbe hai viliumbwa na kitu, jambo au nguvu yenye akili.
Wataalamu wa mabadiliko nao wanapinga na kusisitiza kwamba nadharia yao ni ya kisayansi na ya wale wanaopinga ni ya kidini.

Hivi sasa hata wale waumini wa nadharia ya mabadiliko iliyoasisiwa na Charles Darwin wameanza kuitilia mashaka nadharia hiyo kiasi cha kuitupilia mbali ili kutafuta nadharia mbadala.

Kwa mfano, Mwanabaiolojia mashuhuri kutoka nchini Sweden, Sren Lvtrup, ameweka wazi kwamba, anaamini siku moja nadharia hii ya Darwin ya mabadiliko itakuja kuwekwa wazi kwamba ni nadharia ya uongo kupita kiasi katika historia ya sayansi.

Lakini Nadharia hii ya mabadiliko inaendelea kufundishwa katika mashule yetu ambayo yanahudumiwa na kodi za walalahoi, huku nadharia hii ikiendelea kutiliwa mashaka kila uchao.

Kwa kuwa nadharia ya kidini ina msimamo wake tofauti na ule wa sayansi, sasa kwa nini wanafunzi wasifundishwe nadharia zote mbili, kila moja ikiwa na ushahidi wake ili waweze kupembua ubora na udhaifu wa kila nadharia na kuwawezesha kwa ridhaa yao wenyewe kuamua nadharia ipi kati ya hizo mbili ina ushahidi bora kuzidi nadharia nyingine?

Bado napata kizunguzungu katika kujadili hii mada, kwani kila ninavyozidi kutafuta ukweli nakutana na nadharia zinazopingana, ingawa kila moja haitoi ushahidi unaojitosheleza.

Je wenzangu mnayo maoni gani juu ya hili?

Nahisi mada hii inaelekea kunishinda, naomba msaada wenu.

9 comments:

  1. mjadala huu ni mzuuri na mtamu, sipo katika mazingira ya kuchangia chochote kwa sasa niko bize labda kesho au keshokutwa nitakuja na yangu pia!

    ReplyDelete
  2. Karibu sana Kaka Kamala!! nasubiri kwa hamu mchango wako.

    ReplyDelete
  3. Ahsante dada Yasinta kwa kuurejea huu mjadala.
    Labda huu ndio wakati muafaka wa kupata majibu ya utata huu.
    Mpaka leo bado nilikuwa natafuta majibu na nimekuwa nikiperuzi mtandao na kusoma vitabu mbalimbali lakini nazidi kuchaganyikiwa

    ReplyDelete
  4. Nitarudi, kila jibu nalotaka kulitoa, naona halitatosha kwa sasa, naperuzi kwanza!

    ReplyDelete
  5. Kila mtu na fani yake, mi hii topic imenipiga chenga mazima. Lakini kudesa ruksa, naingia chimbo kuperuzi. Ntarejea, haijalishi ni lini?

    ReplyDelete
  6. Mimi ni mtalamu kiasi wa sayansi, sijihusishi kabisa na anthropolojia ambayo kwa kiasi fulani huangalia vionjo vya kale. Ukiwasikiliza hao watu wanadai mwanadamu wa kwanza au wa zamani zaidi alikuwa Afrika, tena wanasema ya kuwa waafrika au watu weusi wamekabiliana na mabadiliko mengi sana ya kimaumbile kuliko watu wa asili nyingine YOYOTE, kwa mtazamo huo, basi wazungu au wahindi bado wanafanana au wako karibu na nyani kuliko waafrika!
    Waafrika kwa rangi ya uso wanakaribia kufanana na nyani, lakini kwa nywele, hapo ni wazunu au wahindi nk.
    Vinasaba, nyani ni tofauti kabisa na binadamu, ingawa binadamu wote kwa vinasaba tuko sawa.

    Kwa hitimisho, hakuna binadamu aliyebadilika kutoka katika aina yoyote ya nyani au sokwe!!

    ReplyDelete
  7. haya na mimi sasa natoa mtizamo wangu.

    kwanza yawezekana kabisa kuna binadamu wengine tofauti na tuwajuao katika ulimwengu usioonekana!

    nakubaliana kidogo na mtizamo wa binadamu alikuwa nyani. kumbuka kuna wanyama wafananao kama vile nyani, ngedele, sokwe mtu, tumbili, binadamu nk.

    inasemekana na labda hii ni kweli kuwa binadamu wa kale aliishi juu ya miti. alipogundua moto ndipo akaanza kuishi mapangoni kwani moto ulimsaidia kufukuza wanyama wakali. kwa hiyo kiumbe aliyeishi juu ya miti ni mnyamatu! baadaye ubunifu ukaendelea akaanza kujenga vibanda kujikinga na jua na mvua na ndo akaja kugundua nyumba nk, nk nk

    binadamu anabadilika na anaendelea kubadilika. ukimuona mzee wa zamani na wewe ngozi zenu zi tofauti. tunazidi kuwa mayai na kufa kwetu kunaongezeka kuliko zamani.

    nadhalia ya evolution nikubalianayonayo na ili ya uumbaji zinafanana. kwa nini mungu amuumbe adamu na hawa pekee na asiendelee kuumba mpaka leo hii? pia haiingii akilini kuwa adamu na hawa walifanya ngono na kutuzaa sote.

    ukitembelea maajabu kama vile amboni caves utaona jinsi dunia ilivyobadilika. nadahria ya uumbaji na ile ya evolution zinafanana kwani zote zinaonyesha ujio wa mimea kabla ya binadamu.

    rangi za binadamu zisikusumbue hasa wewe unayeamini katika uumbaji. maumbile yaliumba kwa makusudi rangi hizi. rangi na lugha ni sawa. Maumbile (mungu) yaliumba rangi ili kupendezesha nchi au macho yake. hii ni sawa na mpaka rangi. siku zote mpaka rangi huwa na makopo tofautui ili kupendezesha ukuta. nyumba za rangi zote ni sawa na zote ni nyumba na ndivyo ilivyo kwa binadamu. wote tu sawa japo rangi ya ngozi yetu ni tofauti lakini roho au injini ya maisha ni moja! ndio maana hakuna daktari asomeaye kutibu waafrika au wahindi au wachina kwani waote tu sawa na ukisomea udaktari umeusomea na unawatibu wote bila rangi kwa sababu sote tu wamoja. ndio maana Yasinta umeolewa na mswidishi kwani viungo vyote vya ngono vinaingiliana tu na ubora ni ule ule.

    lugha tofauti nazo ni kama mziki. ndi maana kwaya huwa na sauti ya kwanza, ya pili, ya nne nk, nk illi ufyatuke wimbo mwema. Mungu akisikiliza maongezi yetu kwake ni mziki wa kufa mtu kwani una kila miksi ya sauti na lugha nk, wale mnaofanya sound meditation mnaelewa haya.

    binadamu kufananishwa na mapanya na manyani hii ni sawa. hatuhitaji kuamini kuwa binadamu alikuwa panya au nyani, bali tunapaswa kuona umoja uliopo kati yetu na wanyama hao. sisi na wanyama ni kitu kimoja. tofuti ni kuwa sisi tuna mwili wa akili (mind) unaotufanya kuwa watundu na kuishia pabaya. vinginevyo ukiangalia anatomi yetu ni moja na ndio maana tunashairiwa au tunapaswa kutokumla mnyama yeyeto kwani ana uhai kama sisi na ni sawa na kujila sisi wenyewe.

    futailia maisha ya akina kristo uone walikula nini, buddha, mohammad, ng'wanamarundi, nk.
    kula nyama kulikua kama tambiko la kijinga pamoja na uchoyo wa binadamu. hata biblia kwa wanaoiamnini, hairuhusu kula nyama. kasome mwanzo 1:29 uone chakula ulichopewa na warumi 14:21 uone juu ya nyama. kwa hiyo sisi na wanyama hao ni wa moja na ndio maana kuna wanaodhani tulibadililka, hapana. sema sisi tuna utashi na tunafikiri. utashi huu na kufikiri vimetupeleka pabaya sana kuliko pazuri!

    ndo hayo tu,nadharia ya uumbaji na evolution zinafanana ukiziangalia kwa ukaribu.

    ReplyDelete
  8. Kamala asanteni kwa mchango wako Kama nilivyosema kila kitu kwangu kilikuwa gizani.Sasa naanza kupata mwanga kwani umeeleza kwa kirefu kiasi kwamba mtu unaelewa.

    Shabani nimefanya hivi kwani najua wote tunataka jibu na tupo pamoja.
    Mwanasosholojia ninaimani utarudi na jibu nzuru nawe Fadhy pia nakusubiri ila fanyeni haraka:-)
    Dada Mariam kweli Mmmhh mmhhh ni kweli kwelikweli

    Chib asante sana kwa maoni yako yamekuwa na msaada mkubwa.

    ReplyDelete