Kuna tabia ya sisi wazazi kuwaahidi watoto kwamba tutawapa zawadi fulani kama watafanya kitu fulani. Tatizo la kwanza linalojitokeza hapa ni kwa mtoto kushindwa kujua kwamba anapaswa kufanya mambo mazuri hata kama hakuna zawadi.
Kila wakati mtoto atakuwa akifanya jambo au mambo mazuri kwa matarajio ya zawadi na endapo kutakuwa hakuna zawadi hataona sababu ya kufanya hivyo
Mtoto anapoambiwa kwa mfano kwamba akiwa wa kwanza darasani atapatiwa viatu, anakuwa anajengewa dhana kwamba viatu sio haki yake bali ni mpaka afikie matarajio fulani ya mzazi wake ili aweze kupata viatu.
Kuna wazazi ambao huwaahidi watoto wao zawadi kama nguo, midoli, baskeli na vitu vingine vinavyofanana na hivyo, ambavyo kimsingi ni haki yake.
Wengi wetu tumelelewa katika mazingira ya aina hii. Tulipokuwa wadogo wazazi wetu walishindwa kujua kwamba viatu, nguo, midoli na kadhalika ni haki yetu, bila kujali kama tumefanya vizuri darasani au tumefanya jambo lolote tulilopaswa kulifanya kwa ustadi mkubwa, kama walivyotarajia.
Kwa mtindo huo wa malezi wametufanya tuamini kwamba ili tupate haki zetu ni lazima tufikie matarajio ya wazazi.
Na sisi tumejikuta tunatumia mbinu hiyo hiyo katika kuwalea watoto wetu.
Je? malezi ya aina hii yana athari gani katika ustawi wa watoto wetu?
Labda hilo niwaachie wasomaji mtoe maoni yenu, kwani mimi hili linanitatiza….
ndio, kumpa mtoto motisha ni muhimu lakini motisha au zawadi usifanane au kuendana na vile vitu ambavyo ni haki yake ya msingi kuvipata kutoka kwako ila zawadi kubwa na ya kwanza ni kumpongeza na kumtia moyo na mengineyo
ReplyDeleteKamala umesema kweli kabisa.
ReplyDeleteLabda niontoe mfano mmoja:- Unajua kuna wazazi wengine kwa kutaka mtoto afanye kiti kwa mfano kufanya usafi chumba alalacho anamwambia ukifanya utapata zawadi.