Friday, June 5, 2009

CHIMBA KISIMA CHAKO MWENYEWE By Faustin Munishi:


Uchimbe kisima wewe mwenyewe unywe maji yako peke yako na usiyashiriki nao wengine ni hatari kubwa eeh!
Maji ya kisima cha watu wengi yameingiliwa na mdudu ukiwa na kiu usiyaonje utaambukizwa eeh.
Na kiu ya maji imeongezeka watu wanayanywa kila wakati na yanauzwa kote barabarani nani atapona eeh?
Kwa sababu maji yana mdudu yanapatikana kirahisi ukipita kote utayaona wacha kuyachota eeh.


Ukiwa na njaa ni ya chakula huwa ni vigumu upatiwe lakini sigara na hata pombe watakupatia eeh.
Unajua kwa nini?
kwa sababu pombe na sigara zinaua wanataka na wewe ufe na wao wanakupatia eeh.
Tena na siku hizi na hayo maji yaliyo yaliyoingiwa na mdudu utapewa bure bila kuomba ili mfe wote eeh.
Yapo kwenye chupa kubwa na ndogo watu wanazipenda zile ndogo wanafikiliria zipo salama wamedanganyika eeh.
Wanazifunika nusunusu wamefanya hivyo makusudu ili waamushe kiu ya maji usidanganyjike eeh!

Ndugu jihadhari na maji ya rahisi kachimbe kisima wewe mwenyewe ukiwa na kiu uyanywe maji uliypoyachimba heri.
Dawa ya mdudu hawajaipata wanaitafuta kotekote umwamini Yesu akuokoea amalize kiu

Unaweza kusikiliza wimbo hapa chini



Mithali 5: 15 – 19
Unywe maji ya birika lako mwenyewe, na maji yenye kububujika kwenye kisima chako.
Chemichemi yako ibarikiwe nawe umfurahia mke wa ujana wako!

Asante Kaka Lazarus Mbilinyi

5 comments:

  1. Ujumbe muruuuuua!mwenye masikio na asikie, mwenye macho na aone, mwenye pua na anuse! Thanks dada Yasinta na Kaka Mbilinyi!

    ReplyDelete
  2. Nilipoanza kusoma post hii nikawaza ningetoa poetic comments, lakini nilipomaliza nikajikuta nimenogewa, nikashiba na hatimaye kuvimbiwa. Hamu ya ushairi ninayo tena?
    Maji ya kisima. Yawe yangu mwenyewe! Kazi kweli kweli. Unajua nini? Visima vyenyewe havina mifuniko. Unaweza ukaenda kazini ama safarini, mpumbavu (ama tuseme mwendawazimu) mmoja akakutilia hiyo sumu.
    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  3. Masikio na macho yanapata vionjo vingi, bila kuwa na hayo masikio na macho, nafikiri tungekuwa ma mbumbumbu wote. Ujumbe nimeuona na kuusoma, masikio yamesikia wimbo.
    Nimekubali

    ReplyDelete
  4. Tutakaokufaidi maji ya Uzeeni kazi kwetu!

    Kheri yao wasioogopa kufa!

    ReplyDelete