Thursday, March 12, 2009

MJADALA WA LEO:- KWA NINI WATU TUTOE RUSHWA

Kichwa kinaniuma sana kila nikifikiria hili jambo la rushwa. Najua mtasema nimesahau mambo yanavyokuwa nchini mwangu. Labda NDIYO:- Ni hivi juzi tu nimetoka nyumbani Tanzania. Kusema kweli nilishikwa na butwaa, kwanza kabisa ni hivi baba yangu amestaafu mwaka juzi 2007. Amepata kiinua mgongo chake, na baada ya hapo inabidi apate (mafao) pesa kiasi fulani kila baada ya miezi mitatu. Lakini mpaka leo hizi za kila baada ya miezi mitatu hajapata. Kila akifuatilia kwenye maofisi yanayohusika wanamwambia njoo kesho au anayehusika hayupo. Yaani hapo wanachotaka babangu awape ya SODA kidogo wakati anataka HAKI yake. Je? hii ni haki kuwasumbua watu/wazee walioitumikia serikali?

Bado sijamaliza:- Jingine ni kwamba mimi ni mgonjwa nahitaji matibabu. Cha kushangaza unaambiwa nipe ya kula mchana. Kwa nini mimi nimpe ya chakula wakati yeye analipwa mshahara. Ndiyo, labda ana mshahara mdogo. Maa sasa inaonekana usipokuwa na refa basi huwezi kufanikisha kitu.

Swali:- Kwa nini inakuwa hivi? na kwa nini isiwe kinyume?

5 comments:

  1. NIMEPENDA THE WAY YOU WRITE AHSANTE KWA KUNIELIMISHA..bra jobbat

    ReplyDelete
  2. Karibu sana Nuru the light. Du är välkomna alltid. Tack att du besökte mig

    ReplyDelete
  3. Yasinta,naomba umuulize mzee wako,yeye alipokuwa akifanya kazi hakuwahi kuomba rushwa?Asije akawa analalamika kuwa mazao ni mabaya wakati mbegu alisaidia kupanda.

    ReplyDelete
  4. Rushwa inapokomaa kuwa sehemu ya kiutamaduni, hatuwezi kupambana nayo kwa njia za kipolisi.

    Rushwa, kwa jinsi ilivyokomaa, tunahitaji kuandaa kizazi kipya kisichopenda rushwa. Tuanze kwa kupanda mbegu njema kwa wanetu.

    ReplyDelete
  5. Katawa babangu alikuwa mwl. naamini hajawahi kuomba /kuombwa rushwa namfahamu babangu.

    Bwaya ni kweli kabisa inabidi tuwe makini sana ili jamii hii changu isiige jambo hili. Unajua mimi nilitaka kumkatalia dr. kumpa pesa ndipo anipe huduma.

    ReplyDelete