Friday, March 27, 2009

MAISHA BAADA YA KIFO

Nimesoma mjadala uliowekwa na Shabani Kaluse uliokuwa na kicha cha habari kisemacho "BADO WATU WANA HOFU JUU YA KIFO" Nami nimeona niendeleze mjadala huu kwa mada hii.

Baada ya kifo kinatokea nini?
Kuhusu kifo kuna mitazamo mbalimbali inayotofautiana kadiri ya imani ya mtu. Katika maisha ya binadamu kwa kipindi chote cha maisha yake, amakuea akipambana vikali sana na swali hili: “Baada ya kifo changu kitaendelea nini?” Jibu la swali hili lina maana sana katika maisha yetu hapa duniani, ingawa watu wengi wanaogopa kuongea juu ya jambo hilo. Madhehebu mbalimbali ya dini yamekuwa yakitoa majibu ya swali hili kadiri ya imani ya mapokeo yao.
Wakristo wanaamini nini?
Lakini katika imani hizo zote, tumaini la wakristo ni la uhakika kwa sababu kuu mbili. Moja, Ufufuko wa Kristo na Pili ni ushuhuda wa Maandiko Matakatifu. Biblia inatupatia picha ya kweli na kamili kuhusu kitakachoendelea baada ya kufa. Hata hivyo, wakristo wengi wameelewa vibaya juu ya maisha baada ya kufa. Wengine wanaamini kwamba watakuwa miongoni mwa malaika, wengine wanaamini wataingia katika hali ya usingizi wa roho, wakati wengine wanaamini kwamba watakuwa wanaelea katikati ya mawingu.
Wakristo wanaamini kwamba Kifo sio kitu cha kuogopa, badala yake katika kufa ndipo tutafikia kilele cha maisha yetu yaani kurudi kwa Baba Mbinguni. Kuishi maana yake tunadumu katika nchi ya kigeni. Kifo kimepoteza maumivu yake na sasa kifo ni ushindi kupitia Ufufuko wa Yesu Kristo Bwana wetu.
Wakana Mungu(Atheists)
Wakana mungu(Atheists) wanaamini kwamba mtu akifa ndio mwisho wake. Hakuna maisha baada ya kifo wala kwamba kuna roho ambayo inakwenda Mbinguni na itaendelea kuishi milele. Tunachotakiwa kutegemea maishani ni kwamba kifo hakiepukiki, binadamu lazima afe na maisha ya ulimwengu huu yana mwisho.
Wale wanaoabudu miungu(Pantheistics) wanafundisha kwamba mtu yumo katika mzunguko usio na mwisho na umwisho mpaka mzunguko huo unapovunjika ndipo mtu anakuwa kitu kimoja na mwumba wake. Namna mtu atakavyokuwa katika maisha ya baadaye inategemea namna gani aliyaishi maisha ya awali. Pale mtu anapounganika na muumba wake, palepale anakoma kuwa kuishi kama mtu, ila anakuwa sehemu ya nguvu za maisha matakatifu kama vile tone la maji linalotua Baharini.
Wale wanaoshikilia dini za makabila yanayosema kwamba vitu vyote vina roho(animistic) wanaamini kwamba baada ya kifo roho ya binadamu inabaki ardhini au inasafiri kwenda kuungana na roho zilizotangulia za mababu (wahenga) zilizoko duniani. Kwa milele wanatembea na wanatangatanga katika giza wakikumbana na furaha na huzuni. Baadhi ya roho hizo zilizotangulia zinaweza kuitwa tena kuja kusaidia na kuwatesa wale wanaoishi duniani.
Waislamu wanaamini nini?
Waislamu wanafundisha kwamba, mwisho wa dunia, Mungu atahukumu maisha na kazi za bainadamu. Wale ambao matendo yao mema yanazidi matendo yao mabaya wataingia paradizini. Wanaobaki wataingia ahera. Korani inafundisha kwamba paradizini watu watakuwa wanakunywa divai na kuhudumiwa na wasichana wa mbinguni na baadhi ya wasichana hao watakuwa wake zao.

9 comments:

  1. Mambo kwenye profile yoko unasemasio tofauti na wewe!
    Nini maana yake na kwani bado ni sawa mpaka leo?

    ReplyDelete
  2. Nina maana mimi ni sawa na wewe au kama wewe.Na ndio bado mpaka leo!!

    ReplyDelete
  3. Dada Yasinta,

    Ahsante kwa kuendeleza mjadala, Ukweli ni kwamba ziko nadharia nyingi juu ya kifo, ulizotaja ni chache sana, lakini hata hivyo nakupongeza kwa kutujuza kile unachokifahamu, ila bado nasisistiza kuwa hakuna haja ya kukiogopa kifo.

    ReplyDelete
  4. Dada Yasinta Utafiti mzuri sana.
    Ahsante kwa kutuhabarisha

    ReplyDelete
  5. Watu wengi wanaogopa sana kifo na sababu kuu ni kwamba wanaogopa maisha baada ya kifo yatakuwaje. kwa Wakristo na Waislam wanaamini kwamba baada ya kifo kuna maisha ya pepo na jehanamu.

    Marastafarian wanaamini kwamba roho haipotei na haifi bali inaishi milele katika namna tofauti tofauti, kwa maana ya kwamba ukifa leo mtu basi unaweza kuzaliwa panya india na kule ukifa utazaliwa maua sehemu nyingine na kule ukifa basi utakuwa simba mbugani yaani wewe utabadilika tu namna lakini lazima uwe hai kama kiumbe

    ReplyDelete
  6. Nimekusikia Shabani "hakuna haja ya kukiogopa kifa"

    Digna, asante na karibu sana hapa kibarazani kwangu.

    Bennet nawe unakaribishwa sana tena kwa mikono miwili.

    ReplyDelete
  7. tafuteni kitu wahindi wakiitacho karma, harafu jua juu ya nguvu juu.

    lingenisheni mambo ya kikirsto juu ya Mungu mwenye upendo wa mwingi anayetushauri kuwapenda mpaka maadui zetu, lakini yeye siku ya mwisho atakuja kuwahukumu na kuwadhibu waetnda dhambi. sasaupendo wa kumpenda adui ni upi? hata hivyo kuna kitu kinaitwa incarnation

    ReplyDelete
  8. Marehemu baba yangu mdogo, aliwahi kuniambia kuwa, yeye haogopi kufa, maana iwe isiwe, ni lazima atakufa. Alichosema anakiogopa yeye ni kutangulia tu, na kuwaacha wanaompenda wakimlilia.

    Rafiki yangu mmoja ambaye wakati huo alikuwa kanali wa jeshi, lakini hivi sasa ni luteni kanali, naye akaniambia kuwa yeye haogopi kufa, bali kinachomuogofya, ni ule mchakato wa kufa.

    Mimi binafsi nadhani niko mkondo mmoja na ule wa baba yangu mdogo hapo awali. Kuogopa kutangulia.

    wajua maandiko yanatuambia kuwa, ukifa, unakufa kimwili, lakini roho inaendelea kuwa hai, na wapo wanaokazia kuwa, roho za wafu baadhi ya nyakati huwatembelea hata ndugu zao majumbani mwao, bila wao kujua. Sasa hapa ndipo penye kasheshe.

    Aisee, hebu chukulia kuwa umetangulia, umeacha vitegemezi na kiburudisho au viburudisho vyako duniani, uliwaandalia mazingira mazuri ya kuishi, mlisota nao sana tu kwenye kuchuma, unapoondoka wewe, ndugu, jamaa na wapuuzi wengine wanatokea na kuwapora kile ulichokuwa umewaandalia. Unapowatembelea unawakuta wanaishi kwa taabu na vilio vya maisha magumu kila siku, huku kile mlichochuma au ulichowachumia wakifaidi wengine. Unaweza kujua uchungu unaoweza kuupata hapo?

    Ndio maana naogopa kutangulia kwakweli.

    ReplyDelete
  9. Duniani kuna nadharia nyingi sana juu ya kifo,kama alivyosema Kaluse.
    Kkubwa ni kuelewa maisha ya hapa dunia yana mwisho kama yalivyokuwa na mwanzo,ila kinachokufa ni mwili tu.Nadhani dini zote zina amini hivyo kuwa kuna maisha baada ya maisha ya hapa duniani.
    Hofu nyingi za watu juu ya kifo sio kutangulia au mchakato wa hicho kifo,wengi wanaamini kuwa baada ya kifo kuna kuadhibiwa na kuchomwa moto na hii inatoakana na matendo yako hapa duniani.Ukweli wengi wakifika hapo HOFU hujaa sana.

    ReplyDelete