Wednesday, March 25, 2009



Ukiridhika na ulichonacho basi utaona maisha hayana ugumu.

13 comments:

  1. Det är sant Jasinta! Jag älskar din blogg förresten. Du beskriva ganska dagliga handelser på en mycket enkelt och förståeligt sätt :D Det gör att jag reflektera vad det är som är meningen med livet ...

    Nitaendelea kupitia!

    Serina.

    ReplyDelete
  2. Är du svensk eller vad kul:D Oc tack så mycket att du tycker om min blogg.

    Na Serina, karibu sana tena na tena!!

    ReplyDelete
  3. Nej, jag är inte svensk men tycker om språk... tänkte brter mönster lite här om det är ok med dig annars kan jag skriva på swahili:)
    Jag är bara blygsam med mina kommentär ... annars smygläser jag varannan dag :) Nu skall alla undrar vad vi snackar om... två afrikanska kvinnor som skriva på svenska...lol

    ReplyDelete
  4. Dada Yasinta, nakuonea wivu unavyotema kiSwidi kama maji :-)

    Mimi ni mtafiti. Siku zijazo, huenda nikakuomba unitafsirie hadithi moja mbili za kiSwidi.

    Una bahati sana ya kujua lugha nyingi, maana nahisi kiIngereza unakijua, Kiswahili unakijua, na kiNgoni ndio unakitafuna kama muwa :-)

    ReplyDelete
  5. Frof Mbele, nasikia Da' Yasinta kasahau kingoni!

    Da Yasinta Umenikumbusha nilipoenda kijijini kwa mama yangu huko upareni, baba aliwawekea wakwe zake Sola ili wasipate tabu ya kutumia vibatari na kandili lakini we! kila mtu na asili yake, pamoja na sola lakini vibatari ilikuwa kama kawa, si unajua mazoea......

    ReplyDelete
  6. Prof. Mbele Bila wivu hakuna maendeleo. Na hizo hadithi hakuna shida naweza nikajaribu kutafsiri usihofu.

    Koero, Ndiyo mazoea hujenga tabia.

    ReplyDelete
  7. Habari za hapa dada Yasinta mwana wa Ngonyani.

    Nimepita hapa kibarazani kwako kujitambulisha kuwa nimefungua kijibaraza changu kitakachokuwa kikijihusisha zaidi na masuala ya vijana.
    Nimekuwa nimsomaji wa blog yako kwa muda mrefu, na sasa nimeamua na mimi nijitose uwanjani ili kuongeza mchango katika kuielimisha jamii.
    Niko ntayari kuelimishwa na kukosolewa pale nitakapoonekana natoka nje ya mstari.
    Natarajia ushirikiano wako.

    Digna

    ReplyDelete
  8. Sehemu kubwa ya watanzania ndiyo maisha yao.Takwimu zinaonyesha kuwa wanaotumia umeme ni asilimia kumi tu.
    Da Yasinta unanikumbusha enzi zile nilipokuwa na zamu ya kuwasha kandili.
    Ukweli ndiyo huo kitu chochote ukikubaliana na ukweli wake maisha huwa ni matamu sana.
    Da Yasinta mgeni amepiga hodi Tumkaribishe.

    ReplyDelete
  9. Oh! kumbe tumepata mgeni karibu sana katika dunia ya blog Digna na karibu sana kibarazani kwangu. Tupo pamoja.

    Nuru. kweli maisha ni matamu hizo zamu za kuwasha kandili hata hazihesabiki. Na Nuru asante kwa kunikumbusha tayari nimeshamkaribisha mgeni:-)

    ReplyDelete
  10. Bila kuridhika ni ulafi.
    Hakuna kuridhika pasi na furaha.
    Furaha hailetwi na fedha.
    Furaha huja kwa kujua kusudio la maisha.
    Ukilijua, waweza kuwa na furaha kuliko mwenye umeme.

    Kwani kwanini twafanya kazi?
    Si kusaka furaha? Ama kuna kingine?

    ReplyDelete
  11. Hii imetulia sana,hapo huna hata presure ya kulipa bill's,maisha yanakwenda kiulaini kabisa kama kumsukuma mlevi, hahahaa inapendeza sana.

    ReplyDelete
  12. Kaka Bwaya, nakubaliana nawe ni kweli bila kuridhika hakuna furaha. Sikujua kuwa nawe ni mwanashairi:-)

    DADA, PASSION4FASHION.TZ ni kweli tulipokuwa Ruhuwiko maisha yalikuwa swali hakuna wa kukusumbua kulipa bili kwani tanesco ni yako. ha ha ha raha kweli na pia kazi kwelikweli

    ReplyDelete