Thursday, December 11, 2008

VIAZI VITAMU (MBATATA) = UTAMU


Chips ya mihogo, chips ya viazi vitamu kwa kachumbali hicho ndio kilikuwa chakula changu. Yaani basi tu. Asante Fadhy Mtanga kwa kunikumbusha kuhusu vyakula hivi.:)

8 comments:

  1. Dada Yasinta,
    Mbona unatutamanisha namna hiyo!!!!!!!
    Nimemisi kweli Viazi vitamu, ngoja leo nikavitafute na kesho jumamosi, itakuwa kaaaaazi kweli kweli.
    Jamani si mnajua raha na karaha ya viazi vitamuuuuu....
    Hasa ukivila usiku.

    ReplyDelete
  2. Shabani! Ebu Niambie raha na kalaha ya viazi vitamuuuuu....umesema Hasa ukivila usiku.

    ReplyDelete
  3. Aaaah Yasinta wewe ni mtu mzima.
    Unataka uelezwe kila kitu?

    ReplyDelete
  4. hapo kunakitu mnatuficha kuhusu usiku maana usiku una negatives nyingi. mimi simo na nasema simo!

    ila umenikumbusha mbali, sisi tulichemshiwa na maganda yake tukala asubuhi kama kitafunwa. inasemekana ndio maana nina akili nyingi.

    ila picha hii ukiiagalia vibaya utadhani umeend kinyume na "maadili" na kuweka picha zisizostahili kuwekwa hadharani za kiume.

    lakini bado ni viazi tu

    ReplyDelete
  5. inategemea kama unaamini una akili kwa sababu ya kula viazi na maganda yake basi amini hivyo. kwani binafsi naamini nina akili kwa sababu nilikula mno vichwa vya samaki.

    Na kuhusu hivyo viazi vinaonekana kama vitu vya kiume. Sikuwaza kabisa hivyo. Naona umeenda mbali mno. utajiju Kamala na mawazo yako. Kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  6. Nyie wananchi! Mwenyewe nloomba viazi nipo. Attention please...viazi vitamu ni vitamu tena vinaleta hamu havihitaji kitunguu saumu kukupa wazimu wa kibinadamu mwulize hata mwalimu hakukwepa majukumu ndo maana una elimu ya kuitumia humu.
    Nilinogewa na viazi vitamu nikaanza kughani.
    Hayo mengine ya vinaonekaje mi simo jamani.!
    Da Yasinta wakati ukisoma Majengo primary kuna mwalimu wa kike aitwa Gauza unamnyaka?

    ReplyDelete
  7. Karibu sana Fadhy viazi nimekuletea. Pia samahani sikusoma pale majengo shule ya msingi isipokuwa nilisoma kuwa typist pale kwa Peter Mgao.

    ReplyDelete
  8. jamaa kaka kalama acha kabisa hakuna ubishi hapa, tena namuunga mkono dada Yasinta a.k.a. KANYANJA yaani KICHWA cha samaki kina akili sana, ndiyo maana hata mgomo pale mlimani nashiriki eboooooo!!! Yaani unidagadisi kweli namuyaku, mwenga kazi kwelikweli. Yaani ukila kichwa cha samaki unapata akili sana hasa yale MANDONGO, umesahau dada Yasinta? unakumbuka kapili? mweeeeeeee. wewe nyasa nyasa nyasa ni zaidi ya yote bwana. oooooooh nakupenda sana nyasa

    ReplyDelete