Saturday, December 13, 2008

FARAJA YA MALAIKA(MAISHA)

Wakati unahitaji faraja ni ndipo uhakika wa maisha yako yanakuwa na muda,
Tafuta uhusianao kwa malaika wa faraja yako,
Mpe jibu hata kama mefumba macho.

Malaika mlinzi anakulinda,
Kila kitu kitaenda safi kwako.
Hakuna mwingine zaidi ya yeye,
Yupo kila mahali bila kusemas kwa heri.

Anatusikia wote na kutuona.
Unatakiwa kusema kwa sauti yako,
Usiwe na wasiwasi na ukawa mzigo kwako,
Uwe na imani kuwa kuna mtu atakufariji.

WIKI END NJEMA PIA JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!!

4 comments:

  1. Ahsante sana da Yasinta. Nimefurahia sana. Nami nakutakia wikend njema. Usisahau kwenda kanisana kesho.
    Alamsiki.

    ReplyDelete
  2. hapana sitasahau, kwani kumshukuru mungu ni lazimi kwa hiyo kesho nitaenda kusali.

    ReplyDelete
  3. Jamani nilikua nje ya kijiji chetu hapa nyasa maana kazi za kuvua siyo mchezo. Lakini nimerudi hapa kwenye bandari kuu naona maneno ya FARAJA matamu kuzidi asali ni raha sana. kweli Salini rozari ili mpate amani ya kweli kwani alisema yeye ndiye njia ya uzima wa milele, atakaye msadiki hatakuosa utakatifu wake na atamweka mkono wa kuume.
    Dada Yasinta Upo mtu wangu??? lakini tabasamu la kwenye picha safi na maneno safi. ubarikiwe na lihimidiwe jina la bwana. JUMAPILI NJEMA

    ReplyDelete
  4. kwa nini unamwita malaika? kwanini huwa watu hasa waafrika wanaenda kanisani?
    hivi tusioenda kanisani tunakosa nini kizuri? kukumbushwa kama tuna dhambi au?

    ReplyDelete