Friday, December 5, 2008

UNDUGU WA NAMNA TOFAUTI KWA MANUFAA YA JAMII

Nitajaribu kidogo kuelezea Ninakotoka mimi vipi tunaitana

Babu - Bibi

Upande wa mama
Mama
Mama mdogo, mdogo wa mama
Mama mkubwa, dada yake mama
Mjomba kaka ya mama

Upande wa baba
Baba
Baba mdogo, mdogo wake baba
Baba mkubwa, kaka yake baba
Shangazi, dada yake baba.

VIPI KUITANA
Watoto wa mama mkubwa na mdogo
Wa kike nitamwita dada au kama ni mdogo basi mdogo wangu
Wa kiume nitamwita kaka hata kama ni mdogo
Watoto wa mjomba ni binamu zangu

Watotot wa baba mkubwa na mdogo
Wa kiume nitamwita kaka naye ataniita dada
Wa kike nitamwita dada, naye ataniita mdogo wake inategemea nani mkubwa
Watoto wa Shangazi ni binamu zangu

Watoto wa kaka zangu wataniita mimi Shangazi na watoto wa wadogo zangu wa kike wataniita mimi mama mkubwa.
Watoto wa binamu wataniita mimi mama na kaka zangu baba.

Mama na baba yangu watawaita watoto wangu wajukuu na wao watawaita wazazi wangu babu na bibi.

Watoto wangu watawaita kaka zangu wajomba

Bibi ya mama/baba yangu mimi nitamwita mama na babu ya mama/baba nitamwita baba.

Naomba kama nimesahau kitu basi tusaidiane.

Sasa nina maswali:- Je? mke wa mjomba ni mjomba pia? na je? mume wa shangazi ni shangazi pia?

8 comments:

  1. mke wa mjomba ni shangazi na mume wa shangazi ndio mjomba!! Habari ya wenga binti nyasa.

    ReplyDelete
  2. Ramadhani karibu sana kijijini kwangu:- Asante kwa kunitembelea na pia kunitaka hali mimi mzima(nene namzima wenga) Ninakotoka mimi mke wa mjomba ni mjimba pia na mume wa shangazi shangazi pia. Ila imekuwa inanitatanisha sana kumwita mke wa mjomba mjomba na tata zaidi kumwita mume wa shangazi shangazi. Kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kuwa yote haya yategemea watoka wapi. Kwingine mke wa mjomba ni MKAZA MJOMBA na najua kiswahili chake fasaha chakaribiana na hili jina.
    Asante Yasinta kwa kuifanyia kazi CHANGAMOTO niliyoomba kuianika hewani.

    ReplyDelete
  4. Asante kwani ulinipa moyo na nikaona niifanyie kazi mara moja kabla sijasahau. Asante tena.

    ReplyDelete
  5. mimi niko na swali tafadhali mtoto wa binamu yako unaweza ukamuoa tafadhali naomba

    ReplyDelete
  6. Assalaam alaikum wa rahmatullahi wa barakatuh!wapendwa nashkur kwa majibu mloyatowa, ila mimi bado nna swali kuhusu namna ya kuitana!mimi na jamaa tumeowa uwa mmoja!yaani mke wangu na mkewe ni mtu na Dada!sisi waume zao tutaitanaje?

    ReplyDelete
  7. En hee na vipi mtoto wa shangazi yake mama angu namuita nani? Maana mpk hapo huyu shangazi mama kwangu ni bibi

    ReplyDelete
  8. Na je mke wa binamu yangu nitamuitaje?

    ReplyDelete