Wednesday, December 31, 2008

NIMEFIKA SALAMA

Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kunilinda mimi na familia yangu katika safari hii ndefu. Tumefika salama mpaka hapa Dar, safari bado inaendelea. Yaani mpaka Songea kama mnavyojua natoka Songea mngoni. Raha sana kuwa nyumbani joto, watu wachangamfu halafu nyumbani ni nyumbani. Leo sisemi kazi kweli kweli ila nasema raha kwelikweli.

Kwa hiyo napenda kuchukua nafasi hii kwa kuwatakieni wootee HERI SANA KWA MWAKA MPYA 2009. Ila mimi nafaidi zaidi kwa wale wote waliokuwa kwenye nchi za baridi. Ha, ha, haaaaa.

11 comments:

  1. Karibu sana nyumbani. Pia heri ya Mwaka Mpya wa 2009

    ReplyDelete
  2. Asante sana Fadhy, ila joto kali kweli naoga kama samaki.

    ReplyDelete
  3. Faidi tu Dada. Una haki maana umejifunga kibwebwe kufanikisha safari yako.
    Baki salama pamoja na wote huko.
    Upendo kwenu

    ReplyDelete
  4. salam from khudori. you can read my post by Google translate in my site

    ReplyDelete
  5. Heriya mwaka mpya pia..

    usichoke kublog natumaini utatuleta picha za kitonga..

    usafiri salama na mfike salama..

    heri ya mwaka mpya

    ReplyDelete
  6. Dada Yasinta, Karibu sana Nyumbani na ninakutakia heri ya mwaka mpya wewe na familia yako.

    ReplyDelete
  7. Duu ilikuwa RAHA sana pale mahali au vipi dada Yasinta!!! lakini nashukuru umerejea nyumbani kula dagaa, nilifurahi kukutana na kubadilishana mawazo ya blogu au vipi mkuu! salamu kwa wotee.

    ReplyDelete
  8. Dada yangu Yasinta karibu nyumbani suala la joto kama ulivyosema nyumbani ni nyumbani tunakukaribisha kwelikweli.

    Umeonaje mabadiliko ya Tz watu walivyowakarimu? ni hayo tu dada yangu mengi tutahabarishana natumai tuko pamoja na Mungu aendelee kukujaria wewe na familia yako.

    ReplyDelete
  9. Safari njema. Tafadhali tuletee picha nyingi sana za kunyumba.

    ReplyDelete
  10. Karibu sana Yasinta. Ila muhimu, usiache kublogu tafadhali.

    ReplyDelete