Friday, January 9, 2009

SONGEA

Raha kwali kuwa nyumbani sasa nimekuwa hapa nyumbani kwa muda wa wiki moja. Na nimekula kila kitu ambacho sijala kwa muda mrefu. Ila kwa sasa nina kazi kidogo ninapaka rangi nyumba na pia kupanda miti jana nilipanda miti ya kawaida 120 na miti ya matunda pia. Jua kali na joto kweliiiiiiii. Ila ni raha sana kuwa nyumbani.

PIA NAPENDA KUWASHUKURU WOTE KWA KUNITAKIA SAFARI NJEMA ASANTENI SANA.

7 comments:

  1. Dada Yasinta,
    Hongera sana kwa kula kila kitu ambacho hujala kwa muda mrefu, naamini baada ya mwezi utakuwa na figure nzuri zaidi yenye afaya.
    Pia hongera sana kwa kupanda miti 120.

    Upendo daima

    ReplyDelete
  2. hongera sana dada Yasinta (kingonni tunasema Yasinda). hongera pia kwa kupanda miti, miti ni uhani wanasema wataalam. usinisahau nilikuagiza chigoma, na udagala wa kunywanja.

    ReplyDelete
  3. angalia usije ukapatwa na ugonjwa matumbo maana ukizidisha tu heeee

    ReplyDelete
  4. poa nakupongeza kwa kuendelea kushambuli chakula cha asili

    ReplyDelete
  5. Safi sana,nimefarajika kuona upo nyumbani. Zaidi unatumia muda wako vizuri kwa kuboresha mazingira ya nyumbani kwao kwa kupanda miti. Hongera sana kwa hilo.

    ReplyDelete
  6. we kula tu kila kitu si vyoo vipo hata kama sio vya kuflash?

    lol

    ReplyDelete
  7. Karibu sana, home sweet home kumbuka.

    ReplyDelete