Mwenzenu leo nimepatwa na kichaa au sijui nisemeje : Yasinta ni jina langu, nataka kuwaambia ya kwamba jina Yasinta nalipenda sana. Nalipenda jina langu halafu napenda sana watu wanaponiita Yasinta napenda sanaaaaa. Napata shida kidogo ninapokuwa Tanzania wote wanasema Mama fulani au Nangonyani kiasi kwamba nasahau naitwa nani. Ila hapa Sweden wote wananiita jina langu lakini wananiudhi wanatamka vibaya wanatamka na H. Hyasinta. oooh wananiudhi sanaaaaaaa. Ila wao waninijibu ni kwamba wanaposema Hyasinta wanawaza au moja ya ua ambalo linaitwa Hyacint huwa linapatikana sana hapa wakati wa Noel.
Ni hili ua liitwalo Hyacint
Kuna rafiki yangu moja anaitwa Yasinta. Ila yeye huandika Hyasinta. Any difference? Mimi nilidhani maana yake ni ile ile!
ReplyDeleteUna jina zuri sana dada. Hongera. Jivunie jian la Kiafrika.
Nimefurahi kutembelea blogu yako.
Hyasinya?????? siyo sahih kwani matumizi ya lugha yangongana kabisa. ila kiswahili na mengineyo ni Yasinta hta ikiwa kikoloni sawa. unajua wabongo wanapenda mambo au kufanya mambo pasipo kujihoji maana halisi. nakubaliana na dadangu Yasinta ndiyo sahihi kabisa wasiotaka wajinyonge
ReplyDelete@Anon hapo juu: Nimekuelewa. Nadhani kuanza na 'H' ni kukosea. Ladha ya jina zuri kama hili inapotezwa kabisa.
ReplyDeleteNi sawa na kusema eti na mimi nianze leo kujiandika Bwayah, au Buayah.
Nampongeza Yasinta kwa kuliandika kwa silabi za kiswahili sanifu.
Nani nalipenda Sana jina langu Yasinta
DeleteYasinta forever
ReplyDelete