Thursday, September 25, 2008

SWEDENI/TANZANIA

Waswidi ni watu wa ajabu sana sio wote baadhi. Kwa kawaida wao ni watu wakimya sana. Hawapendi kuongea kama Wabongo(TZ) Ukiwakuta waswidi katika kituo cha basi au sehemu nyingine, kitu ambacho wataanza kuongea ni habari za hali ya hewa. Wao ni watu maalum kidogo. Mara ya kwanza nilipata shida sana, lakini huu ni utamaduni wao.

Waswidi ni wabinafsi sana kila mtu na kitu chake/mali yake, kila mtu na mama yake, kila mtu na baba yake, kila mtu na dada/kaka yake, kila mtu na mtoto wake na kila mtu na kazi, pesa, nyumba yake hakuna kabisa ushirikiano kama Afrika yetu. Kila mtu na lake/Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyeweeeeee.

2 comments:

  1. labda watakuelewa wewe kwakuwa uko ughaibuni. wabongo tunadhani ughaibuni kila kitu poa. someni niliyoandika katika blogu yangu

    ReplyDelete
  2. Jamani ughaibuni kila kitu sio poa ni maisha ya bajeti sana kwani huku hadi udogo wa kupandia maua unanunuliwa na nguo ndo msiseme kwani kuna misimu minne joto, joto wastani, baridi na baridi sana. sasa fikiria unahitaji nguo za jotona baridi pia viatu sio kama bongo T-shirt na jeans mambo poa. au sisi akina dada gauni au sketi na pia tunahitaji sandosi. lakini hapa lazima viatu vikubwa na soksi. sipendi soksi lakini inabidi nivae pia kofia kazi kweli mhh mie naipenda TZ yangu na nipo katka harakati za kurudi. mnaotaka kuja ughaibuni kazi kwenu.

    ReplyDelete