Friday, September 26, 2008

JAMII YA WASUKUMA!

MAANA YA NENO WASUKUMA Wasukuma ni mkusnyiko wa makundi madogomadogo kutoka maeneo jirani , na kwamba kundi kubwa zaidi likiwa limetoka Kusini mwa eneo hili la mkoa wa Mwanza.Jina hili limetokana na neno SUKUMA maana yake wa lugha ya Kisukuma na Kinyamwezi KASKAZINI, yaani moja wapo wa ya pande nne a dunia yetu. Wanyamwezi ambao lugha yao inafanana sana na Kisukuma hutuita sisi tulio Kaskazini mwao "Bhasukuma" yaani watu wa KASKAZINI. Nasi huwaita "Bhadakama" yaani watu wa KUSINI.
Tangu siku zote, wasukuma na wanyamwezi walijulikana kuwa wao ni "Bhantu" na kutokana na neno hilo kumekuja kujulikana kundi linaloitwa WABANTU. Kundi hili mara zote limetambulikana kwa lugha wanayozungumza ya KIBANTU. Hivyo, Wanyamwezi, Wakimbu hadi Wabemba walioko Zambia ni kundi kubwa la wabantu kufuatia lugha wanazozungumza.
Taarifa zingine kuhusu chimbuko la wasukuma kutoka kwenye mtandao wa internet…kwenye anwani hii.www.mwanzacommunity.com.org




Katika picha mwenye koti jeusi ndiye mzee mwenye miaka 114 ajulikanaye kama Mzee mtalimbo. Ni mganga wa kienyeji ana wake 7 watoto 14 na wajukuu 82. Mtoto wake wa kwanza ana mika 72.



Hii ni nyumba ya mzee mtalimbo ndani pia ni maazi ya nyuki ambao ni mali yake.




Nahisi hapa ni mke na mume katika safari ya kwenda shambani. Kuwajibika kwani bila kulima hakuna kula.

1 comment:

  1. Nina suala moja kwa wasukuma linanitatiza,ni kuhusu mahari.Ukitaka kuoa lazima utoe mang'ombe mengi tena kama binti ni mweupe basi unaweza kukosa mwana.

    ReplyDelete