Monday, August 18, 2008

AGOSTI 18,2008 KUKUMBATIANA (A HUG)

Leo nimeamua kuandika swala la kukumbatiana:-

Kukumbatiana ni aina ya kugawana furaha na uchungu. Wote tunahitaji kukumbatiana kwa sababu tunajaliana. Kuanzia bibi mpaka yule umpendaye. Kukumbatiana ni kitu cha kustaajabisha (kizuri). Ni njia nzuri ya kuonyesha upendo bila kutumia maneno. Ni ajabu kuona kukumbatiana kunawapa watu furaha. Kukumbatiana kunafaa kila mahali kwa lugha zote. Kukumbatiana hakuhitaji betri. Kwa hiyo sasa inachobidi ni kuendeleza mkumbato na mpe/wape rafiki zako na yule umpendaye. Haya mimi nanza tayari sasa hivi nimesha kukukumbatia. :-)

2 comments:

  1. Duh..ebwana hii imekaa njema sana.

    Hakika suala la kukumbatia kama ulivyoeleza lina umuhimu mkubwa sana katika maisha yetu.

    Achilia mbali kuna baadhi ya tamaduni za watu au mifumo ya malezi waliyokulia bado hilo suala hawajalipokea kama ni suala la kimaadili wanachukulia ndivyo sivyo.

    Mwisho wa siku mtu akikuta unamkumbatia ze mai waifu inakuwa kizaa zaa...

    Safi kwa kutumbusha jinsi ya kupeana nguvu katika maisha yetu

    ReplyDelete