Mpaka leo ni miaka minne (4) imepita tangu mama yangu mpendwa Alana magnus Ngonyani aiage dunia hii. Ila kwa mimi inaonekana kama ilikuwa jana tu. Napenda kukuombea mama kwa sara hii:-
Salamu, Maria, umejaa neema,
Bwana yu nawe,
umebarikiwakuliko wanawake wote,
Na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
Utuombee sisi wakosefu,
Sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
Marehemu astarehe kwa amani, Amina.
Pole Yasinta kwa kuondokewa na mama mpendwa.
ReplyDeleteKumbuka sisi wote ni wasafiri katika dunia hii.
Kikubwa tuzidi kumuombea mwenyezi Mungu aiweke roho ya mama mpendwa mahala pema peponi.Amina
Raha ya milele umpe ee bwana..na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani.Amina.
Kikubwa ni kuendeleza yale mema aliyokuwa anafanya.Sisi wote ni wasafiri siku moja nasi tutaiaga hii dunia.
Hongera Yasinta kwa kuwa na blog nzuri kama hii.
Siku njema
asante sana kaka Edwin kwa kutembele blog yangu pia maoni yako mazuri. Nimefurahi
ReplyDeletePole sana dada Yasinta,
ReplyDeleteNi kweli inaumiza sana kupotelewa na mama mzazi, hata hivyo kila roho iliyoumbwa itaonja mauti, hivyo jambo la msingi ni sisi tuliohai kujiandaa kwa ajili ya kifo siku tukiitwa.
Mungu akupe faraja Kuuu