Haya sasa wasomaji leo nimekumbuka Geografia kidogo.
Litumbandyosi ni kijiji ambacho kipo katika kata ya Litumbandyosi. Tarafa ya Namswea. Wilaya ya Mbinga na mkoa wa Ruvuma. Kijiji hiki kipo kusini magharibi mwa Tanzania. Mashariki kinapakana na kijiji cha Mgazini ,Magharibi kinapakana na kijiji cha Rwanda, Kaskazini kimepakana na kijiji kiitwacho Kingoli na kusini kimepakana na kijiji cha Luhagala. Litumbandyosi ni maarufu kwa kilimo cha mpunga, karanga na mihogo. Kijiji cha Litumbandyosi kina jumla ya watu 7,318 na idadi ya kaya ni 1,449 na kila kaya kwa wastani wanaishi watu watano.
Kijiji hiki ndipo alipozaliwa baba yangu.
Na; Yasinta Ngonyani
shibe shibe....haina bei....naenda kula nyumbani.... inanogaaa.. kwani nyumbani ni nyumbani....hata kama kichankani....ama kweli nyumbani ni dhahabu
ReplyDeleteYafaa kujua historia na chimbuko La kijiji Chetu na lugha halisi ya wanalitumba
ReplyDelete