Gazeti la mwananchi hapa sweden limeandika hivi:.
Johannesburg: Siku chache zilizopita mageto mengi ya huko Johannesburg yameongua moto kwa fujo kali, kwa sababu ya kufukuza wakimbizi, hasa wakimbizi wa kutoka Zimbabwe. Ma mia ya mapolisi wameitwa huko getoni Alexandra, ili kujaribu kuwatuliza watu ambao wanatoka nyumba hadi nyumba. Wanafanya hivyo kwa ajili ya kuwasaka wakimbizi. Majambazi wanapowakuta waamiaji hao wanawaibia mali zao, wanaunguza nyumba zao na kuwapiga wananchi. Kesi nyingi za vifo na ubakaji (mzito) mbaya umeripotiwa lakini hata hivyo haijulikani wangapi wamekufa.
Wanazimbabwe mamia kwa mamia wamekimbia na kutafuta njia ya kwenda katika vituo vya polisi ili kuepuka uwingi wa watu.
Na; Yasinta Ngonyani
Habari hii imenuuma sana roho, kwa nini tusiokoana sisi kwa sisi. Yaani wana wa Afrika na Afrika yetu. Tushikamane na tuwe na amani.
ReplyDelete