Friday, May 16, 2008

Mei, 16,2008 BABA

Naona hapo http://www.lundnyasa.blogspot.com/ ananilaumu kwa nini sijampa baba sifa. Hapana kwani bila baba basi basi tusingezaliwa. Kwani lazima tukumbuke Mungu alimuumba Eva lakini baadaye aliona si haki Eva awe peke yake alimletea mume Adam. Nadhani wote mmenielewa. Kwa maana hiyo baba naye ana sifa zake, ambazo hazifanani na mama kwani, Kama mmewahi kumsikiliza Dr Remmy Ongala anavyoimba kwa kweli unaweza kulia. (baba amepata mke mwingine na wangoni kwa ugimbi). Hii ndio sababu niliandika kwanza mama na ukizingatia kwa sasa mama yangu mpendwa hayupo nami. Pia mama ana majukumu makubwa zaidi yaani ana kazi ya kuzaa, kulea, na kazi za aina mbalimbali za nyumbani. Inawezekana labda nilikuwa namtamani mama. Kwa hiyo msidhani ya kwamba simthamini/ sina upendo na baba HAPANA. Si unajua father and dotter. natumai nimewapa wasomaji jibu la kuwapendeza.

Na; Yasinta Ngonyani

1 comment:

  1. aaaaaa jamani nani alianza adamu au eva?Dada mmh kumbe mnajipendelea eeeh?.Sawa lakini ngoja niwape somo wasomaji,hivi nani bora kati ya baba na mama?.pia nisahihishe kidogo lwani dada amesahau herufi moja ni

    http//;www.lundunyasa.blogspot.com

    ReplyDelete