Monday, May 12, 2008

Mei, 12, 2008 Dini/wakoloni

Hii habari nimetaka muda mrefu kuieleza lakini nilikuwa nashindwa vipi nitawaeleza watu sasa nimepata njia ya kuelezea kwa kifupi. Ni hivi;. Hapo kale Waafrika tulikuwa na nchi pia dini zetu yaani tulikuwa tunajitawala pia tulikuwa na dini zetu. Lakini baadaye wazungu wakaja na kutawala afrika, kwa unyonge wetu tukakubali kutawaliwa. Pia walipokuja wakaja na dini zao. Wakatuambia tuache dini zetu za kuamini mizimu na wakaanza kujenga makanisa na kuanza kuhubiri. Hapo ilikuwa mwaka 1898-1998 kama umesoma (UJIO WA WAMISIONARI WABENEDIKTINI TANZANIA - UNGONI) Na sisi kwa unyonge na upole wetu tukawaamini. Nadhani tangu hapo akili zetu zinaamini wazungu wanaweza kufanya kila kitu tunawaheshimu wao kama mungu. Jambo ambalo si kweli. Ninachotaka kusema ni kwamba wazungu /wamisionari walipoingia afrika waliingia kwa kasi na kuanza aina ya vita yaani kuonyesha wao ndio wenye nchi. Pia wao waliona ni jukumu lao kutusaidia waafrika. Hii ndio sababu mpaka leo tuna kaa tu na kusubiri kupewa ( asante baba) yaani kupata miasaada. Bado inanitatanisha sana, Kwani waafrika bado tunaamini yote tuliyofunzwa na wazungu. Hususani dini, wakati wao wenyewe wameacha kabisa kuamini kuwa kuna MUNGU wanaamini miungu wengine kama miti n.k. Je? kwa nini wao walitukataza sisi tusiamini miungu/mizimu wetu?

Na; Yasinta Ngonyani

No comments:

Post a Comment