Kama ulisoma blogg ya hali ya hewa ya kwamba kulikuwa na baridi kiasi kwamba mtu hukuweza kutoka nje. Sasa ni kinyume kabisa watu wamefufuka. Kiasi kwamba unashikwa na butwaa kuona watu jinsi wanavyojianika kama mihogo. Kwa kweli mila na desturi ni kitu muhimu sana. Siku ya kwanza nilishikwa na butwaa kuona baba, mama, mtoto, mamamkwe, babamkwe wote wamejianika kama mihogo au mamba. utakuta wtu wanatembea na hizi nguo za kuogelea siku nzima. Kisa wanataka kupata rangi yaani sisi binadamu hakuna anayeridhika na kile mungu alichompa. Mwafrika anataka kuwa mzungu na mzungu anataka kuwa mwafrika.
Na; Yasinta Ngonyani
Binafsi sipendi kukua juani na ninaipenda rangi yangu. Yaani kuwa mwafrika.Kwa nini kubadili rangi
ReplyDelete