Saturday, May 10, 2008

Mei 10, 2008 kazi bila mshahara

Hakuna mtu apendaye kufanya kazi bila kulipwa,kama si utumwa. Kwani nimesoma na pia nimesikia hapa na pale ya kuwa kwa sasa kuna utata wa walimu Afrika(tanzania) kuna shule moja ipo hapo Songea inaitwa Taifa foundation sec. school. wao hawana walimu. Inawezekana wakawa siku nzima bila kupata hata kipindi kimoja. Walimu wamekula mgomo hawapati mshahara. Ni vizuri kwa wao na ni hasara kwa wanafunzi. Kwani ukizingatia kuna wanafunzi ambao wanahitimu yaani kidato cha nne . Inaonekana watu wanadharau sana kazi ya ualimu na wanasahau ya kwamba hatuwezi kupata elimu bila ya walimu na walimu hawawezi kufanya kazi bila kupata ridhiki yao. Cha kushangaza zaidi ni kwamba wanafunzi wakifanya maandamano/kulalamika, hakuna anayewasikiliza isipokuwa wanapigwa marungu na wengine hata kuwekwa ndani je? Wanafunzi hao hawana haki? Na ukizingatia hiyo elimu si bule, kwa hiyo sio walimu tu ambao inabidi walipwe. Kwani hata wazazi wanaumia wanatoa ada ili watoto wao wapete elimu. Kama itaendelea hivi basi hakutakuwa na taifa la kesho. Je? wasomaji mnasemaje labda inawezekana Waziri wa Elimu halifahamu suala hili au vipi. wani inabidi lichukuliwa majukumu haraka sana tunapoteza maraisi, mawaziri na maprofesa wa baadaye.

Na; Yasinta Ngonyani

No comments:

Post a Comment