Kwa muda mrefu nimekuwa ninajiuliza kwa nini watu Ughaibuni wanakuwa na haraka. Maana utakuta mtu ana kitabu napia kalamu, humu ndani ya kitabu ameandika kila kitu nani atakutana naye leo au atafanya nini siku hii, yaani kuanzia asubuhi mpaka jioni. Nimejaribu kuwauliza kwa nini wanafanya hivi? wengine wanasema bila kufanya hivi basi hawawezi kuishi. Pia nimejaribu kuwaambia nitakako mie hakuna mambo haya yaani kwa mfano, naenda kumsalimia mtu/jamaa au rafiki ni kwenda tu na pia wakati huu nakwenda naweza nikakutana na rafiki /mtu mwingine na hapo gumzo litaanza. Lakini hapa haiwezekani kwani safari imepangwa kwenda kwa (Anna). basi ni kwa "Anna". Kwa hiyo sasa utakuta hata watoto wadogo wanasema hawana hali nzuri kwa vile wana mambo mengi. Mambo mengi kiasi kwamba wengine wanashindwa kuendelea na masomo vizuri. Kwa ajili ya (Stress) KILA KITU NI MUDA HATA KULA CHAKULA. Pia hata kutembea. Ammmh kwa kweli naipenda Afrika yangu hakuna haraka afrika au mie mwongo semeni mwenyewe basi kama kweli au vipi.
Na ; Yasinta Ngonyani
hii kali ya miaka nenda rudi,ndiyo maana wanaumwa sana ugonjwa wa kukosa furaha huku wakijitibu wkidhani ni matizo ya homa za kawaida kumbe ni hayo hayo.hapa Mlimani tunao lakini afadhali kwani naona wanaoana tabia za kiafrika ni nzuri japo yanwashinda
ReplyDeletehao jamaa wanakaribia kushi dunia ya vichaa haki ya mungu wala situkani.ukuiona mtu anafanya hivyo hata kama leo naenda kumsalimia baba aua mama na kule akaingia jikoni kupika basi aseme nimepika kwa baba na mama
ReplyDelete