Matunda ni kutoka nje na kuchuma, kama muonavyo ni papai, passion, tunda damu, machungwa na ndizi. Raha tupu-:)
Chai kwa vitumbua...nimekumbuka enzi hizo ili kupata pesa ya kalamu basi tulikuwa tukipika vitumbua.
Saturday, June 29, 2019
Monday, June 24, 2019
TUANZE HII WIKI NA PICHA HII KUWA IWE PICHA YA YA WIKI ...
Pamoja na kuwa amebeba mtoto na mzigo kichwani lakini sura yake ni ya furaha ...nimeipenda hii picha...
Monday, June 17, 2019
HODI HODI NYUMBANI ....RUVUMA YITU YABWINA
Kwetu ruvuma ni kuzuri nje kuona na mahindi mje kula vyakula vya asili . KARIBUNI SANA MAANA MIE NISHA KARIBIA:-)
Wednesday, June 12, 2019
NIMEAMKA NA WAZO HILI LEO
Nawaza kwa sauti kwa nini mifuko ya plastiki inakatazwa lakini sio viti vya plastiki. Maana ukiangalia hiki kiti kina ubora zaidi kuliko cha plastiki...nimewaza tu kwa sauti
Sunday, June 9, 2019
TUFANYE NYUMBA ZETU KUWA "KIJIWE" CHA MARAFIKI WA WATOTO WETU
nimekumbuka enzi zilee
Siku zote fungua milango kwa watoto kufurahi nyumbani kwako na watoto wenzao na utawasaidia kuepuka mengi kwa dunia ya sasa yenye changamoto za kila namna. Ni vyema mtoto akawa huru kuchagua rafiki, ila kama mzazi / mlezi unaweza kumsaidia ushauri tu juu ya marafiki wema wenye maadili mema kama wewe ulivyojitahidi kumfundisha. Sikiliza mazungumzo yao, michezo na tabia za marafiki aliowachagua mwanao kisha umshauri kuhusu marafiki hao endapo utaona sio marafiki wazuri na mpe pongezi unapoona marafiki zake ni binadamu wema. Ni vyema pia ukayafanya makazi yako kuwa sehemu rafiki kwa marafiki wa watoto wako kujumuika na kufurahi pamoja. Hii itakusaidia kujua tabia za marafiki hao na pia itasaidia kuwaweka salama watoto wako kwa sababu watacheza na kufurahi nyumbani kwako na sio sehemu zingine usizofahamu