Sunday, June 9, 2019

TUFANYE NYUMBA ZETU KUWA "KIJIWE" CHA MARAFIKI WA WATOTO WETU



nimekumbuka enzi zilee
Siku zote fungua milango kwa watoto kufurahi nyumbani kwako na watoto wenzao na utawasaidia kuepuka mengi kwa dunia ya sasa yenye changamoto za kila namna. Ni vyema mtoto akawa huru kuchagua rafiki, ila kama mzazi / mlezi unaweza kumsaidia ushauri tu juu ya marafiki wema wenye maadili mema kama wewe ulivyojitahidi kumfundisha. Sikiliza mazungumzo yao, michezo na tabia za marafiki aliowachagua mwanao kisha umshauri kuhusu marafiki hao endapo utaona sio marafiki wazuri na mpe pongezi unapoona marafiki zake ni binadamu wema. Ni vyema pia ukayafanya makazi yako kuwa sehemu rafiki kwa marafiki wa watoto wako kujumuika na kufurahi pamoja. Hii itakusaidia kujua tabia za marafiki hao na pia itasaidia kuwaweka salama watoto wako kwa sababu watacheza na kufurahi nyumbani kwako na sio sehemu zingine usizofahamu

No comments:

Post a Comment