Friday, March 30, 2018

IJUMAA KUU HII IWE NJEMA KWA WAUMINI WOTE!!


Ni ijumaa ambayo Bwana Yesu Kristu atapata mateso kwa ajili yetu. Sijui kama kuna mtu angeweza kujitoa roho yake kwa ajili ya mwingine kama Bwana wetu Yesu anavyofanya kwa ajili yetu?..Na nawakumbusheni kuto sahau leo ni ile siku ambayo ni siku moja tu kwa mwaka ambayo tunaombwa kuacha kula vyakula vya damudamu hasa nyama ....Mwenyezi Mungu na atawala Nyumbani mwenu Daima kuwa na Amani pia Furaha . Amina. IJUMAA KUU IWE NJEMA KWA WOTE....  NI KAPULYA WENU!!

Thursday, March 29, 2018

HISTORIA YA ALHAMISI KUU


ALHAMIS KUU KWA WOTE NA TUKUMBUKE KUPENDANA.

Monday, March 26, 2018

USITAFUTE PESA TAFUTA FURAHA

Katika maisha kitu kigumu kuliko vyote kukitafuta sio pesa bali ni furaha. Pesa ni ngumu kuitafuta kwasababu kila siku tunaipoteza katika kuitafuta furaha. Pesa humaliza matatizo na matatizo humaliza pesa. Inawezekana hata aliyezigundua  alikufa na madeni, sioni sababu ya kufa kwa sababu ya kutafuta maisha, bora uzima.  Pesa sio kila kitu. Inaweza kununua nyumba lakini haiwezi kununua familia, inaweza kununua  kitanda lakini haiwezi kununua usingizi, inaweza kunuua saa lakini haiwezi kununua muda. Pesa inaweza kununua vitabu lakini haiwezi kununua akili. Na maskini sio yule tu ambaye hana bali hata yule aliyenazo lakini anazitaka zaidi. Tafuta furaha kila siku usisubiri mpaka muda maalumu ndio uwe na furaha. Kila siku hapa duniani ni siku  maalumu. Na kwa taarifa yako sio mwenye pesa tu anayeweza kuhamisha milima hata fukara kapuku kama wewe na mimi. Pesa sio kila kitu bora furaha, inaweza kununua madaraka lakini haiwezi kununua heshima. Inaweza kununua damu lakini haiwezi kununua uhai, inaweza kununua dawa lakini haiwezi kununua afya. Pesa  haiwezi kununua mapezi.
CHANZO.- NILITUMIA NA RAFIKI KMA VIDEO/SIMULIZI NAMI NIMEUGEUZA KAMA MADA..

Wednesday, March 21, 2018

MAONI YALIYOTOLEWA NA KAKA RAY NJAU KUHUSU TAULO ZA KIKE!


HAPA NI KAKA RAY NJAU 

Kukabiliana na Matatizo ya Kukoma kwa Hedhi

“Ghafula nilihisi nimelemewa na huzuni bila kujua sababu. Nililia na kuanza kujiuliza ikiwa ninarukwa na akili.”—Rondro, * mwenye umri wa miaka 50.

“Unaamka asubuhi na kupata nyumba yako ikiwa shaghalabaghala. Huwezi kupata kitu chochote unachotafuta. Mambo ambayo ulikuwa ukifanya kwa urahisi, sasa yanaonekana kuwa magumu sana, na hujui ni kwa nini hali iko hivyo.”—Hanta, mwenye umri wa miaka 55.

WANAWAKE hao si wagonjwa. Wanapitia tu kipindi cha kukoma kwa hedhi, ambacho ni badiliko la kiasili katika maisha ya mwanamke anapoacha kuwa na uwezo wa kupata watoto. Ikiwa wewe ni mwanamke, je, unakaribia kipindi hicho? Au je, unapitia kipindi hicho sasa hivi? Vyovyote vile, kadiri ambavyo wewe na wapendwa wako mnajifunza kuhusu kipindi hiki cha mabadiliko, ndivyo mtakavyoweza kukabiliana kwa njia inayofaa na matatizo yanayohusiana nacho.
Kipindi cha Kukoma Hedhi

Wanawake wengi huanza kipindi hicho wakiwa na umri wa miaka 40 na kitu, lakini wengine huanza wakiwa wamechelewa wakiwa na miaka 60 na kitu. * Kwa wanawake wengi, hedhi hukoma hatua kwa hatua. Kwa sababu ya kubadilika-badilika kwa kiwango cha homoni kinachotokezwa, huenda mwanamke akakosa kupata hedhi pindi kwa pindi, akapata hedhi wakati ambao hakutarajia, au akavuja damu nyingi isivyo kawaida wakati wa hedhi. Wanawake wachache hukoma kupata hedhi ghafula, yaani, wanakosa hedhi mwezi mmoja na huo unakuwa mwisho wa kuipata.

Kitabu kuhusu kukoma kwa hedhi (Menopause Guidebook) kinasema: “Kipindi hicho huwa tofauti kwa kila mwanamke.” Kitabu hicho kinaendelea kusema hivi: “Matatizo ya kawaida yanayohusiana na kipindi hicho ni kupata joto la ghafula mwilini,” ambalo huenda likafuatwa na kuhisi baridi. Dalili hizo zinaweza kumfanya mtu akose usingizi na kuishiwa na nguvu. Matatizo hayo huendelea kwa muda gani? Kulingana na kitabu hicho, “wanawake fulani hupatwa na joto la ghafula mwilini kwa mwaka mmoja au miwili wakati wa kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi. Wengine hupatwa na hali hiyo kwa miaka mingi, na wachache sana husema kwamba wao hupatwa na joto la ghafula mara kwa mara maisha yao yote.” *

Kwa sababu ya kubadilika-badilika kwa kiwango cha homoni, huenda mwanamke akashuka moyo, hisia zake zikabadilika-badilika na hilo linaweza kumfanya alielie bila sababu, na pia asiwe makini sana na asahau mambo. Licha ya hayo, kitabu The Menopause Book kinasema kwamba “kuna uwezekano mkubwa kwamba mwanamke hatapatwa na mambo hayo yote.” Kwa kweli, wanawake fulani hupata matatizo machache sana na wengine hawapati matatizo yoyote wakati wa kipindi hicho.
Jinsi ya Kukabiliana na Kipindi Hicho

Kubadili mtindo wa maisha kunaweza kupunguza baadhi ya matatizo hayo. Kwa mfano, wanawake wanaovuta sigara wanaweza kupunguza mara ambazo wanapatwa na joto la ghafula kwa kuacha kuvuta sigara. Wanawake wengi hunufaika kwa kubadili mazoea yao ya kula kama vile kupunguza au hata kuacha kunywa kileo, vinywaji vyenye kafeini, na vyakula vyenye sukari au vikolezo ambavyo vinaweza kusababisha joto la ghafula mwilini. Bila shaka, ni muhimu kula vyakula mbalimbali na vyenye lishe.

Kufanya mazoezi husaidia sana kupunguza matatizo yanayohusianishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa mfano, mazoezi yanaweza kupunguza kukosa usingizi na kusaidia kuboresha hali ya kihisia na pia kuimarisha mifupa na afya ya mtu kwa ujumla. *
Eleza Mambo Waziwazi

Rondro aliyenukuliwa mwanzoni mwa makala hii anasema hivi: “Usiteseke kimyakimya. Ukiwaeleza wapendwa wako mambo waziwazi, hawatakuwa na wasiwasi kuhusu hali yako.” Jambo hilo linaweza kuwafanya hata wakuonyeshe subira na huruma zaidi. “Upendo ni wenye ustahimilivu na wenye fadhili,” linasema andiko la 1 Wakorintho 13:4.
chanzo:www.jw.org/sw
Maoni yanatoka katika mada hii TAULO ZA KIKE! kila la kheri kwa wote na ahsante sana kaka RAY.


Tuesday, March 20, 2018

KUMBUKUMBU.....NIMEIPENDA HII PICHA NA NIMEONA IWE PCHA YA WIKI HII

UJUMBE:- JANA NI HISTORIA. KESHO NI MIUJIZA  NA LEO NI ZAWADI.
NAPENDA KUWATAKIENI SIKU YA LEO IWE NJEMA SANA, FURAHA NA AMANIPIA. KAPULYA WENU....

Monday, March 19, 2018

MICHEZO YA WATOTO:- UKUAJI NA MAARIFA WAYAPATAYO....!

 Watoto uwaleavyo ndivyo wakuavyo hapa wakiwa wanacheza bao mchangani....zaidi mchezo huu huchezwa na watoto wakiume....au vijana pia akina baba. Wengi wetu nadhani twaukumbuka mchezo huu...ni mchezo lakini hapo kunamambo wanajifunza kama vile hesabu nk.
 Na hapani watoto wa kike wakicheza mchezo wa mdako... nilipenda sana mchezo huu....maharage yalikuwa yanaungua kila mara :-)
 Watoto wengi hasa wa kiume walipenda sana kucheza huu mchezo kama baiskeli au gari vile ni ringi la baiskel ...hapa watakiwa kuwa na balansi...
Usipojifunza mapishi tangu udogo itakuwa shida...ni mchezo lakini ndiyo kujifunza huko.....zamani watoto walikuwa wakijifunza vitu vingi sana na kupata maarifa ...lakini sasa  mmmhhh wapo mitandaoni tu....

Thursday, March 15, 2018

KUMBUKUMBU:- NIMEKUMBUKA KWETU LITUMBANDYOSI/KINGOLI TULIKUWA TUNAKULA SANA HAYA MATUNDA NA KUCHOMA KOROSHO WENYEWE ILIKUWA SAFI SANA NA TAMU

Korosho na mabibo ya njano
Na hapa ni korosho na mabibo mekundu
Nikukumbuka hii nakumbuka pia mbula zilivyoniponza na nusu ya kupotenza kidole changu kimoja kwa ajili ya kubangua mbura ili kupata zile karanga.....

Tuesday, March 13, 2018

UJUMBE WA LEO TOKA KWANGU KUJA KWENU

Mfanyie mtu mambo/jambo mazuri/zuri na mema akiwa hai, kwa sababu chochote utakachomfanyia aliyekufa hakina maana kwa vile hatasikia.
NAWATAKIENI SIKU NJEMA

Sunday, March 11, 2018

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMAPILI NJEMA SANA

UJUMBE WA LEO:- Katika maisha ni muhimu kuuliza pale unapokuwa na dukuduku  Udadisi  una maana yake.

Friday, March 9, 2018

PALE UPATAPO WASAA WA KUPUMZIKA BASI PUMZIKA KWANI NI MUHIMU KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Hapa yaonekana kuna kitu alikuwa akishangaa  au sijui hakuwa na njaa?
CHAKULA AKIPENDACHO KAPULYA KULIKO VYOTE HAPA DUNIANI NI SAMAKI
BAADA YA KAZI YA WIKI NZIMA SIO MBAYA KUJOPONGEZA KIDOGO. NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA WIKI HII NA IWE YA FURAHA NA AMANI ITAWALE KATIKA KAYA ZENU.

Monday, March 5, 2018

NI WIKI NYINGINE NA NI JUMATATU NAMI NIMEONA TUANZE HIVI.....

Nimekumbuka sana enzi zile ambapo tulikuwa tunakula chakula/vyakula kwa pamoja. Lakini  siku hizi umezuka mtindo wa watu kula chakula kila mtu sahani yake. JE? wewe  hii unakumbuka wapi?

Thursday, March 1, 2018

SWALI LA LEO. .....JE? Ni WAPI KAPULYA WENU YUPO?

Nawatakieni  wote AMANI NA FURAHA ....PAMOJA  DAIMA...KAPULYA